LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakusanyaji taarifa binafsi watakiwa kujisajili PDPC

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Taasisi za Serikali na binafsi zinazojihusisha na ukusanyaji na uchakataji wa taarifa zimetakiwa kujisajili katika mfumo wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), kabla ya tarehe 30 Aprili 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Mkilia ametoa rai hiyo Jumamosi Machi 22, 2025 wakati akizungumza kwenye warsha ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi namba 11 ya mwaka 2022.

Amezitaja taasisi zinazopaswa kujisajili kuwa ni pamoja na zinazotoa huduma za kifedha, vyombo vya habari na watoa huduma za malazi (hotel, guesti & lodge) na kwamba lengo la tume ni kuhakikisha taarifa za faragha za kila mmoja zinalindwa.

Baadhi ya wanahabari jijini Mwanza akiwemo Albert Sengo wamekiri kwamba sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ikisimamiwa vyema itasaidia kulinda faragha za wananchi kwani si kila taarifa zinapaswa kutolewa kwa umma.

Taarifa binafsi za mhusika ni pamoja na jina kamili, kabila, jinsia, namba ya simu, barua pepe, kiwango cha elimu, namba ya hati ya kusafiria, NIDA nk.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia akizungumza jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji PDPC, Mhandisi Stephen Wangwe akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo.
Kaimu Uhusiano na Mawasiliano PDPC, Innocent Mungy akizungumza kwenye warsha hiyo.
Wanahabari jijini Mwanza wakiwa kwenye warsha hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.