LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbio za Utalii Kanda ya Ziwa kufanyika jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya Kilimanjaro One Sports Promotion Limited, imeandaa mbio za utalii Kanda ya Ziwa zinazotarajiwa kufanyika Juni 27-29,2025 jijini Mwanza.

Mbio hizo za kimataifa 'Lake Zone International Tourism Marathon 2025' ni sehemu ya maandalizi kuelekea kwenye tamasha kubwa la kiutamaduni la Kanda ya Ziwa litakalofanyika mkoani Simiyu mwaka huu.

Hayo yamebainishwa Ijumaa Machi 21, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Kilimanjaro One Sports Promotion Limited, Mohamed Khatibu wakati akizungunza na na waandishi wa habari, wadau wa utalii na wanariadha jijini Mwanza.

Alisema utalii wa mbio hizo utajumuisha watoto, wanafunzi, walemavu, wamama wajawazito, makundi mbalimbali ya mazoezi, viongozi wa daraja la kwanza ndani ya Mkoa na Kanda ya Ziwa pamoja na wananchi wote.

"Madhumuni makubwa ya mbio hizi ni kutangaza vivutio vya kiutalii na fursa za kiuwekezaji zinazopatikana katika Jiji la mwanza ili kukuza uchumi wa kanda ya ziwa na Taifa kwa ujumla" alisema Khatibu.

Aidha alieleza kuwa kila uwekezaji wa kiuchumi unahitaji utulivu wa nchi na amani ya watu wake, hivyo watatumia mbio hizo kuhamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha na kushiriki uchanguzi mkuu kwa amani mwezi Oktoba 2025.

Alisema wanakusudia kuwa na zaidi ya washiriki 2,000 katika tukio hilo na zawadi kabambe zitatolewa ambapo zitawekwa wazi rasmi wakati wa uzonduzi hivi karibuni.

Naye Msimamizi Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua alisema watatumia mbio hizo kama mkakati wa kutangaza utalii nchini kupitia michezo huku washiriki wakijiimarisha kiuchumi na kiafya.

"Michezo inaleta watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo pato la mkoa litaongezeka, watu watafanya mazoezi ambapo afya zitaimarika na watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii" alisema Kabarua.

Naye Mtaribu wa Huduma ya Afya ya Uzazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana alisema mbio hizo ni fursa kubwa kwani itawasaidia kuendelea kutoa elimu kwa wajawazito ambayo itasaidia kupunguza vifo kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga.

Alisema katika mbio hizo, wajawazito watashiriki kwa kufanya mazoezi mepesi ikiwemo kutembea kwa dakika 20 hadi 30 hatua itakayosaidia kuimarisha afya zao.

"Kunafaida nyingi za kufanya mazoezi kwa wajawazito ikiwemo kupunguza uzito, kusaidia mzunguko wa damu kwenda vizuri na kupata usingizi mzuri" alisema Yohana.

Mmoja wa washiriki wa mbio hizo ambaye ni mtoto, Amani Issa aliwaomba wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kushiriki mbio hizo ili waweze kuimarisha afya zao.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Kilimanjaro One Sports Promotion Limited, Mohamed Khatibu akizungumzia ujio wa mbio za utalii katika Mkoa wa Mwanza.
Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana akizungumzia umuhimu wa wajawazito kushiriki mbio hizo.
Mmoja wa washiriki wa mbio za kiutalii Kanda ya Ziwa, Amani Issa akizungumza namna alivyojipanga kuwa mshindi wa kwanza upande wa watoto.
Wadau mbalimbali wa riadha jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.