Shirika la WOTESAWA lashiriki maashimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakati mwelekeo wa dunia ukiwa ni kuhimiza usawa wa kijinsia baina katika jamii, shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani WOTESAWA, limesisitiza kuwa usawa huo haupaswi kuwaacha nyuma wafanyakazi hao.
Afisa Ustawi wa Jamii wa shirika hilo, Renalda Mambo ametoa rai hiyo Alhamisi Machi 06, 2025 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa Mwanza katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo kilele cha maadhimisho hayo ni Machi 08, 2025.
Rai hiyo ya shirika la WOTESAWA inaendana na kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji" ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kukuza usawa wa kijinsia, haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: