LIVE STREAM ADS

Header Ads

TPDC, ZPDC zaendelea kushirikiana uendeshaji sekta ya gesi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Februari, 2022 liliingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) ambapo kupitia ushirikiano huo masuala mbalimbali yamekuwa yakifanyika kuiendeleza Sekta ikiwemo kubadilishana ujuzi na utaalam.

Kapinga ameyasema hayo Aprili 14, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwahani, Khamis Yussuf Mussa Mkenge aliyeuliza ni lini Serikali itainufaisha Zanzibar katika matumizi ya Nishati ya Gesi ili iweze kutumika katika magari.

"Mheshimiwa Spika katika ushirikiano huu suala la kupeleka gesi Zanzibar ni mojawapo ya agenda kuu. Pande zote mbili bado zinaangalia namna bora ya kufikisha gesi asilia Zanzibar ili iweze kupatikana kwa bei nafuu kwa watumiaji.". Amesema Kapinga

#KAZIINAONGEA
Kazi na Utu, Tunasonga Mbele!

No comments:

Powered by Blogger.