LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la BabyMoon Africa laja na suluhisho kwa watoto njiti, uzito mdogo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Babymoon Africa limekabidhi mbeleko (Kangaroo Mother Care) ili kuwasaidia wazazi waliojufungua watoto kabla ya muda na wenye uzito mdogo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.

Akizungumza Mei 15, 2025 jijini Mwanza wakati wa maadhimisho ya siku ya Kangaroo Mother Care, Mkurugenzi wa shirika la Babymoon, Albany James alisema mbeleko hizo zinasaidia wazazi na walezi kuwabeba kwa ufasaha watoto hao na hivyo kuimarisha ukuaji wao.

Katika maadhimisho hayo, imebainika kubwa idadi ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda na wenye uzito mdogo inafikia zaidi ya 100 kwa mwezi katika hospitali zote mbili za Sekou Toure na Bugando.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.