LIVE STREAM ADS

Header Ads

JUKWAA LA NNE LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI LAANZA MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini limeanza rasmi leo Juni 16, 2025 jijini Mwanza ambalo linakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wizara ya Madini na Taasisi zake, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Taasisi za Fedha, Kampuni za Uchimbaji wa Madini na Watoa Huduma kwenye Migodi ya Madini.

Jukwaa hilo lenye kaulimbiu inayosema Ongezeko la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ni chachu ya Ukuaji wa Uchumi linaambatana na maonesho yenye lengo la kuelimisha kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Mada zinazowasilishwa katika Jukwaa hili ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini Tanzania; Usimamizi na Uendeshaji Bora wa Kampuni za Ndani ni Chachu ya Ongezeko la Ushiriki wa Watanzania Sekta ya Madini; Mafanikio ya Ubia kati ya Kampuni za Kigeni na Kampuni za Kitanzania na majadiliano kuhusu Fursa, Mafanikio na Changamoto katika Uanzishwaji wa Viwanda vya Kuzalisha Bidhaa zinazohitajika Migodini Nchini.

No comments:

Powered by Blogger.