Kongamano la Dira ya Taifa 2050 na ubia wa maendeleo kufanyika Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kongamano la kitaaluma linalolenga kujadili nafasi ya ubia katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050 linatarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Lupa Ramadhani, amesema kongamano hilo ni hatua ya awali katika utekelezaji wa dira hiyo, likilenga kupanua wigo wa ushiriki wa wananchi katika mijadala ya maendeleo na kuhimiza uwajibikaji wa pamoja katika kujenga taifa.
“Wiki iliyopita, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050 ilizinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo msisitizo mkubwa umewekwa katika nafasi ya ubia. Hili linatokana na malengo ya dira hiyo yanayohimiza ushiriki wa kila Mtanzania katika kuleta maendeleo ya nchi, sambamba na kuzingatia uwazi na utawala bora” amesema.
Anasema kongamano hilo lina umuhimu wa kimkakati kwa sababu linatoa fursa ya kuchambua nafasi ya PPP katika safari ya maendeleo wa taifa ,litabaini changamoto na fursa zilizopo katika mifumo nya sasa ya PPP, litajenga mwafaka kuhusu mikakati ya kuanisha juhudi za PPP na vipaumbele vya Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 pamoja na kuimarisha ushirikianao kati ya sekta ya umma na binafsi katika utekelezaji wa malengo ya taifa.
Aliongeza kuwa lengo kuu ni kukuza uelewa wa pamoja na wa kimkakati wa thamani ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kufanikisha dira ya maendeleo ya Taifa 2050 huku hoja mbalimbali zitashindanishwa na kujadiliwa ili kupanua uelewa na kuwepo kwa lugha moja hivyo hiyo ni fursa kwa wakazi wa Mwanza na Watanzania wote kushiriki kongamano hilo ambalo litagusia maeneo makuu matatu .
“Tutagusia maeneo matatu ambayo ni dhana ya PPP na nafasi yake kuelekea dira ya Taifa 2025 nafasi ya PPP katika kukuza uwekezaji na ufanisi katika uendeshaji wa serikali za mitaa na nafasi ya sekta binafsi na mitaji kutoka nje katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania mjadala huu utakuwa wa wazi na tunatarajia kuwa na washiriki 300 “ameeleza.
Anasisitiza kuwa suala hilo ni la Kitaifa hivyo ili kuhakikisha PPP inachangia ipasavyo katika dira hiyo kunahitajika majadiliano ya kina, miungano ya kimkakati na uelewa wa pamoja baina ya serikali ,sekta binafsi ,asasi za kiraia, taasisi za elimu ya juu na washirika wa maendeleo .
Naye Mkuu wa Kitengo cha habari PPP Chelu Matuzya anaeleza kuwa kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya mpango wa utafiti na elimu ya demokrasia Tanzania na Kituo cha Ubia wa Serikali na Sekta binafsi linatarajiwa kuwa la kipee lenye ushawishi na manufaa kwa taifa lenye mlengo wa kujadiliana kwa uwazi ubia, uwekezaji na mwenendo wa kiuchumi na kisiasa kitaifa na mwelekeo wa taifa katika miaka 25 ijayo na kuhakikisha miradi yote inafanikiwa kwa asilimia 100.
Imeandaliwa na Neema Emmanuel, Mwanza
No comments: