Msigwa atembelea banda la JAB, asisitiza Usajili na Waandishi Watia Nia kujiweka kando
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa akisaini kitabu cha Wageni pamoja na kuzingumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB, leo tarehe 06 Julai, 2025 alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendela katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewasisitiza Waandishi wa Habari nchini kutambua kuwa safari ndefu ya kufikia utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari imelenga kulinda taaluma ya Uandishi wa Habari, hivyo wale waliopo kwenye vyombo vya habari na hawana sifa warudi shule kwani vyuo vipo.
Bw. Msigwa ametoa msisitizo huo leo tarehe 06 Julai, 2025 mara baada ya kutembelea Banda la Bodi la Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB lililopo katika Kijiji cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumza machache na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Wakili Patrick Kipangula.
No comments: