Maonesho ya Nanenane 2025 yahitimishwa kwa kishindo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi maarufu kama Nanenane yamekuwa na mwitikio mkubwa katika Kanda ya Ziwa Magharibi inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.
Maonesho hayo hufanyika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza ambapo kitaifa mwaka yamefanyika jijini Dodoma na kutoa fursa kwa wananchi, taasisi, mashirika na wadau kutoa elimu, kutangaza na kuuza bidhaa mbalimbali.
Tazama picha wakati wa kilele cha maadhimisho ya Nanenane Ijumaa Agosti 08, 2025 katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi ilitoa zawadi za vyeti, vikombe na fedha kwa washiriki waliofanya vizuri kwenye maonesho hayo ambapo kampuni ya DEKALB iliibuka mshindi wa pili upande wa wauzaji wa pembejeo na mbegu za kilimo.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) pia iliibika nafasi ya pili.
Kwa taasisi za elimu, Chuo Kikuu SAUT pia kiliibuka mshindi wa pili.
Upande wa Serikali za Mitaa, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iliibuka mshindi wa kwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: