TAMASHA LA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025 LAFANA JIJINI MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Jumamosi Agosti 23,2025 imeandaa tamasha kubwa kwa ajili ya hamasa ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru utakaowasili Jumatatu Agosti 25,2025.
Wananchi na makundi mbalimbali yameshiriki tamasha hilo lililoambatana na mbio za pole (jogging) katika mitaa ya Jiji la Mwanza na mazoezi ya viungo katika uwanja wa Nyamagana wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Makilagi amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Nyamagana pamoja na kujiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani kama ilivyo kauli mbiu ya Mwenge mwaka huu ambayo ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025, kwa Amani na Utulivu".
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zadi
No comments: