KIZA MAYEYE KUKAMILISHA KITUO CHA AFYA KAGUNGA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mgombea ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Kiza Mayeye ametoa ahadi ya kuhakikisha mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kagunga kinakamilika ndani ya kipindi cha miaka mitano ya ubunge wake iwapo atachaguliwa kuwakilisha jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Akihutubia mkutano wa kampeni Kijiji cha Kagunga, Mayeye amesema kukamilika kwa mradi huo ni muhimu kwa sababu siyo tu itasogeza huduma kwa wananchi, bali pia itaokoa maisha ya wagonjwa, hasa wanawake wajawazito na wanaohitaji huduma za rufaa za dharura.
Kwa sasa wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa za dharura hulazimika kusafishwa kwa kutumia mitumbwi kwa zaidi ya Saa 5 kwa usafiri wa boti kufuata huduma hizo mjini Kigoma.
Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kagunga umefikia hatua ya ujenzi wa maboma na kupaua baada ya Serikali kutoa zaidi ya Sh500 milioni.
Kata ya Kagunga yenye vijiji vitano iko mwambao wa Ziwa Tanganyika na haifikiki kwa njia ya barabara kutokana na ukanda wa milima inayoizunguka.
Usafiri pekee wa kwenda na kutoka kwenye kata hiyo ni wa njia ya maji kwa kutumia maboti.
No comments: