MAONESHO YA KWANZA YA KEKI KUFANYIKA MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maonesho ya keki kwa mara ya kwanza nchini Tanzania yanatarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia Septemba 03- 07, 2025 jijini Mwanza, yakilenga kuwaleta pamoja wadau wa sekta hiyo kubadilishana ujuzi na masoko.
Mwandaaji wa maonesho hayo, Bernard James kutoka kampuni ya BJ Empire amesema sekta ya keki imekuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira hivyo maonesho hayo yatatoa chachu zaidi katika kukuza sekta hiyo.
Bernard ambaye pia mwanahabari, amesema kupitia maonesho hayo, wajasiriamali watapata fursa ya mafunzo, kukutana na wadau wakiwemo wauzaji wa vifaa vya keki pamoja na kutoa fursa ya kukutana na wateja wapya na kwamba hakutakuwa na kiingilio kwenye maonesho hayo yatakayofanyika ukumbi wa “Gandhi Hall”.
Mwandaaji wa maonesho ya keki Kanda ya Ziwa, Bernard James akizungumza na wanahabari.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: