UWADOMAMI WALAANI UCHAGUZI WAO KUINGILIWA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha wajasiriamali katika masoko na minada (UWADOMAMI) mkoani Mwanza, kimelaani mchakato wa uchaguzi wa viongozi wake kuingiliwa katika Wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Wakizungumza wakati wa mkutano mkuu ulioambatana na zoezi la kuwaapisha viongozi wa wilaya za mkoa wa Mwanza ambazo tayari zimefanya uchaguzi, viongozi wa chama hicho wameomba viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa wa Mwanza kuingilia kati mkwamo huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya amesema malalamiko hayo bado hayajafika ofisini kwake ambapo ameahidi kuyashughulikia yatakapomfikia.
Katibu Mkuu UWADOMAMI, David Philipo akizungumza kwenye mkutano wa chama hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Katibu Mkuu UWADOMAMI, David Philipo akizungumza kwenye mkutano wa chama hicho.
Mwenyekiti wa UWADOMAMI Mkoa wa Mwanza, Justine Sagara akiongoza mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: