LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJENZI WA KAMPASI YA NJOMBE UDOM WAANZA KWA KASI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Ujenzi ukienda kwa pamoja na usomaji ramani na michoro. Watalaamu wakiangalia kwa makini michoro ya ujenzi wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi.

Na Mwandishi Wetu.

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Lughano Kusiluka, ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya UDOM mkoani Njombe, huku akisisitiza mkandarasi kuongeza kasi ili mradi ukamilike kwa wakati.

Akizungumza leo Septemba 9, 2025 baada ya kukagua ujenzi huo, Profesa Kusiluka alisema majengo yanapaswa kukamilika ifikapo Mei 2026 kama ilivyopangwa, bila kuongeza muda wa mkataba.

Kwa upande wake, Mshauri Elekezi wa Mradi, Mhandisi Filbert Shayo,amesema kuwa ujenzi umefikia asilimia 15, huku hatua za msingi zikiendelea kukamilishwa.

Kampasi hiyo inatarajiwa kuwa chachu ya kuboresha elimu ya juu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini.


MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Lughano Kusiluka, akikagua kwa makini uchimbaji msingi katika moja wapo ya majengo yanayoendelea kujengwa Njombe.


Mshauri Elekezi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Ujenzi wa Kampasi ya UDOM, Njombe, Mhandisi Filbert Shayo (kushoto) akiwa na Mhandisi Stella Kyabula, Mkurugenzi wa Miliki na Ujenzi, wakikagua maendeleo ya Mradi wakati wa ziara.


Wawawakilishi wa Wananchi waliojumuika na Kamati ya Ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma Njombe, wakikagua ujenzi unaoendelea katika viwanja vya Njosi, Njombe wakati wa ziara ya Makamu Mkuu wa Chuo.


Ujenzi ukienda kwa pamoja na usomaji ramani na michoro. Watalaamu wakiangalia kwa makini michoro ya ujenzi wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi.


Wataalamu wa ujenzi, wananchi na uongozi wa Juu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wakipata taarifa ya maendeleo ya ujenzi unaoendelea Njombe.


Mafundi wakiendelea na zoezi la kusuka Nondo kwa ajili ya Msingi kwenye jengo la Utawala linaloendelea kujengwa.

Mafundi wakiendelea na hatua za ujenzi katika jengo la bweni la wanafunzi, linalojengwa Njombe. Mradio huu unatekelezwa na Mkandarasi Dimetoclasa Realhope Ltd. Jengo hili kwa sasa linaendelea na hatua ya ujenzi wa msingi kama linavyoonekana katika picha.

No comments:

Powered by Blogger.