LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI MKUU AKAGUA KITUO CHA UOKOAJI ZIWA VICTORIA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha kuratibu ufuatiliaji na uokoaji katika ukanda wa ziwa Victoria kilichopo wilayani Ilemela.

Akiongea Ijumaa Januari 23, 2026 na wananchi baada ya ukaguzi huo Dkt. Nchemba amesema Serikali ya awamu ya sita inajali maisha ya wananchi wake na kwamba inajipambanua kwa dhamira ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa hata iliyoshindikana siku za nyuma.

"Jambo hili linahusisha masuala ya kidharula, watendaji kwenye mradi huu msisinzie hata kidogo maana mtaleta maafa kwa kuangamiza maisha ya watu na vifaa vya kisasa vilivyowekwa kwa gharama kubwa kwa fedha ambazo Rais ameweka hapa pamoja washirika wenzetu" Waziri Mkuu.

Naye Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa alisema ukanda wa ziwa victoria umekua na changamoto kubwa ya ajali za majini ambapo takribani watu 20 wamefariki maji na ndipo Serikali ikaamua kuwa na kituo hicho kwa ajili ya uokozi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC), Mohamed Salum alisema Kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kimataifa wa Afrika Mashariki wa kuzuia matukio ya ajali na upotevu wa maisha ya watu ambao uliidhinishwa na Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki mwaka 2007.

Alibainisha kuwa mwaka 2022 hadi 2025 mradi huo ulianza rasmi kutekelezwa kwa pamoja na Mataifa ya Tanzania na Uganda ambapo umelenga kuimarisha usalama wa vyombo kwa kuongeza wigo wa ufuatiliaji wa ajali kwenye vyombo vya usafiri pamoja na wavuvi katika eneo la maziwa.

Alisema kituo hicho cha utafutaji na uokoaji na kupata taarifa halisi za hali ya hewa kwa gharama za Tshs. Bilioni 19.8 kwa upande wa Tanzania huku ikijumuisha gharama za vituo vya Uokoaji vitatu, Boti, Maboya pamoja na jengo katika eneo la kituo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Boti za uokoaji zikiwa Ziwa Victoria.

No comments:

Powered by Blogger.