LIVE STREAM ADS

Header Ads

CP. SHILOGILE AWASILI MWANZA KUFUNGUA MAFUNZO YA POLISI JAMII

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP. Faustine Shilogile, amewasili mkoani Mwanza jumatano Januari 07, 2026, kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kufungua mafunzo ya siku moja kwa Maafisa wa Polisi Jamii kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mafunzo hayo yatahusisha washiriki ambao ni maafisa wa Polisi Jamii kutoka Mikoa ya Mara, Tarime Rorya, Simiyu, Geita, Tabora na Shinyanga.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha mikakati ya kuzuia uhalifu kabla haujatokea na endapo utatokea, usirudiwe tena, kwa mujibu wa mipango iliyowekwa na wadau husika.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama na kuendeleza ushirikiano na jamii katika kudhibiti uhalifu.
Kutoka Dawati la Habari Polisi Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.