FASTJET YAFUNGUA OFISI MPYA AIRPOT MKOANI MWANZA……ATAKAE NUNUA TIKETI KATIKA OFISI HIYO SIKU YA KESHO, KUPATA OFA BABU KUBWA.
![]() |
Wafanyakazi wa FastJet |
Akizungumza
katika Ufunguzi wa Ofisi hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evarist Ndikilo, Kamimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela James Chuwa aliipongeza
Kampuni ya FastJet kwa kurahisisha usafiri wa anga hapa nchini kupitia huduma
zake za Usafiri wa anga.
Aidha Chuwa
alieleza kwamba, pamoja na huduma bora zinazotolewa na Kampuni hiyo bado kuna
baadhi ya changamoto ambazo wateja wa FastJet wanazilalamikia hivyo ni vyema
zikatafutiwa ufumbuzi.
“…Lakini pia
niseme tumekuwa tukikumbana na changamoto mbalimbali ofisini, wananchi wetu
wakitulalamikia… wamekuwa wanasema wamekuwa wanatozwa gharama kubwa sana
kupitia mizigo yao, hilo kwenu lipokeeni kama changamoto na muangalie namna ya
kurahisisha bei ya mizigo…” Alisema Chuwa.
Kwa upande
wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza Easter Madale, aliongeza kuwa suala la
gharama za tiketi za FastJet lingeangaliwa upya ili kiwango cha gharama cha
tiketi za bei ya chini zisiwe na tofauti kubwa na tiketi za gharama ya juu ili
watu wote waweze kunufaika na huduma za Kampuni hiyo ya FastJet.
Pia aliusihi
uongozi wa FastJet kuongeza huduma zaidi katika Ofisi hiyo na kutoa pia huduma
nyinginezo kama vile huduma kwa wateja, badala ya kutoa huduma kwa ajili ya
Mauzo pekee ili kuwarahisishia wateja wake upatikanaji wa huduma karibu zaidi.
Nae Meneja
Masoko wa FastJet Jean Uku aliahidi kuwa Kampuni yake italishughulikia suala la
gharama za usafirisha wa mizigo ya wateja wa FastJet, huku akibainisha kwamba
Mteja atakae nunua tiketi ya Safari siku ya kesho atapata ofa ya kusafirisha
mizigo yake bure kabisa.
“Nimesikia
hiyo na tutaangalia juu ya bei ya mizigo, lakini kwa kuanza kesho tutakuwa na
ofa kwa mteja atakae nunua tiketi FastJet katika ofisi yetu mpya, lakini
pengine in future (siku zijazo) tutapunguza bei ya kusafirisha
mizigo…”.Alibainisha Uku.
No comments: