HOMA YA DENGUE YAGUNDULIKA KUWEPO JIJINI MWANZA.MTUMISHI WA MUNGU AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA MAZINGIRA KATIKA HALI YA USAFI.
Mgonjwa mmoja amelazwa katika
Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekour Tour kwa ajili ya Matibabu zaidi, baada ya
kuthibitika kuwa na Maambukizi ya Ugonjwa wa Dengue unaoenezwa na Mbu aina ya
Aedes.
Akitoa
Taarifa ya Kuwepo kwa Mgonjwa huyo hii leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga aliwataka wananchi Mkoani Mwanza
kuzingatia usafi wa Mazingira sanjari na kuangamiza Mazalia yote mbu katika
mitaa yao ili kujikinga na ugonjwa huo.
Aidha alibainisha
kuwa Ugonjwa huo huwapata watu wa rika zote japo watoto wenye umri chini ya
Miaka Mitano na akina mama wajawazito wana nafasi kubwa ya kuathirika zaidi na
ugonjwa huo wa Dengue.
Taarifa hiyo
ya Konisaga ilieleza kuwa asilimia 90 ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huu
huonyesha dalili za awali kuanzia siku tatu hadi 14 baada ya kuumwa na mbu aina
ya Aedes mwenye maambukizi ya virusi vya vinavyosababisha ugonjwa Dengue.
![]() | |
Mwanahabari Akiuliza Swali juu ya Ugonjwa huo wa Dengue wakati Taarifa ya ugonjwa huo ikitolewa kwa wanahabari. |
![]() |
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Ugonjwa wa Dengue wakati ikitolewa kwao Mkoani Mwanza. |
Miongoni mwa
dalili za ugonjwa wa Dengue ni pamoja na Homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa
hususani sehemu za machoni, maumivu makali ya misuli pamoja na viuongo vya
mwili, kuvimba tezi, kupatwa na harara sanjari na kichefuchefu au kutapik
Asilimia 10
ya wagonjwa wa Dengue hupatwa na dalili kali kama kutokwa na damu kwenye sehemu
za uwazi za mwili kama vile mdomoni, masikioni pamoja na sehemu za siri kama
vile sehemu za haja kubwa na ndogo.
Njia
mbalimbali zinashauriwa kufuatwa ili kujikinga na Homa ya Dengue, njia hizo ni
pamoja na kuzingatia usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na Kuangamiza mazalia
ya mbu kutumia vyandarua sanjari na kutumia dawa za kuzuia mbu.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Kulia Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu), na Mganga wa Mfawidhi Sekour Toure Dk.Onesmo Rwakyendera Kushoto. |
Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Dk.Valentino Bangi alibainisha kuwa mgonjwa huyo alifika
Hospital ya Mkoa Mwanza Sekour Toour jumanne May 20 mwaka huu, na kupewa
matibabu bila mafanikio, ambapo jana aliporudi hospitalini alipigwa kipimo cha
Dengue na kuthibitika kuwa na ugonjwa huo.
“Tarehe 17
mwezi huu mgonjwa huyu ambae ni mstaafu mzee wa makamo mwenye umri wa miakla 62
alienda Dar es salaama katika Hospital Mhimbili-MOI kwa ajili ya matibabu ya
Mifupa na aliporudi ndo alianza kuhisi kuumwa hivyo inaaminika kuwa huko ndiko
alikotoka na maambukizi ya Ugonjwa huo”. Alisema Dk.Bangi huku akisisitiza
zaidi wananchi kuzingatia usafi wa mazingira ili kuangamiza mazalia ya mbu
wanaoambukiza ugonjwa huo.
Katika hatua
nyingine Dk.Bangi alisema kuwa ni jukumu la kila mmoja kujikinga na kujilinda
na maambukizi ya Ugonjwa wa Dengue, ambapo alibainisha kuwa watalaamu wa Afya
Mkoani Mwanza wamejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo,
ambapo mgonjwa hupewa matibabu kulingana na dalili alizonazo kwa kuwa ugonjwa
huo hauna chanjo wala tiba.
“Katika Mkoa
wa Mwanza tumepokea vipimo takribani 50 vya kupima ugonjwa huo, ambapo tayari
kipimo kimoja kimwekwisha tumika hivyo tumebaki na vipimo 49 ambapo baadhi
tumevigawa katika Wilaya za Ukerewe, Kwimba na Sengerema ambapo ambapo hapa
Mkoani Tumebaki na vipimo 20 ambapo Wizara inatarajia kuleta vipimo vingine
katika Bohari ya dawa Kanda ya Ziwa MSD kulingana na Mahitaji kwa kuwa bado
hakuna kasi ya Maambukizi ya Ugonjwa huu”. Alieleza Dk.Bangi.
![]() |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk.Valentino Bangi. |
Kwa upande
wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure Dk.Onesmo
Rwakyendera ambae hakutaka kumtaja mgonywa huyo jina, alibainisha kuwa hatua
mbalimbali zinachukuliwa ili kuhakikisha kuwa kila mgonjwa hospitalini hapo
analala ndani ya chandarua sanjari na kupata dawa kwa ajili ya kunyunyizia ili
kuua mazalia ya mbu hospitalini hapo sanjari na maeneo mengine ya Mkoa wa
Mwanza ikiwa ni pamoja na eneo la Kilimahewa ambapo mgonjwa huyo ametokea.
Kuanzia mwezi
march mwaka Ugonjwa wa Homa ya Dengue ulianza kugundulika Mkoani Dar es salaam
ambapo takribani watu watatu wapepoteza maisha huku wengine zaidi ya 400 wakiwa
wameambukizwa ugonjwa, ambapo sasa ugonjwa huo umeanza kueneo katika Maeneo mbalimbali
hapa nchini kutokana na muingiliano wa watu.
No comments: