LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIONGOZI WA CHADEMA KANDA YA ZIWA KUTINGA MAHAKAMANI, WATOA ONYO KALI KWA WANAOKICHAFUA CHAMA. WAKANUSHA TAARIFA INAYOWAONYA MBOWE NA DK.SLAA KUACHANA NA UKAWA.



Mbowe (Picha Kutoka Maktaba)

Wenyeviti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki, Wametoa onyo kali kwa baadhi ya watu wanaokichafua Chama hicho kwa lengo la kujipatia Umaarufu wa Kisiasa kwa ajili ya Manufaa yao binafsi, huku wakitishia kuwafikisha watu hao Mahakamani.
 

Wenyeviti hao ambao ni kutoka Mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera na Simiyu walitoa taarifa hiyo hii leo Jijini Mwanza, Wakati wakitoa taarifa kwa wanahabari kukanusha taarifa iliyoandikwa na Baadhi ya Vyombo vya Habari kwamba Wenyeviti wa Chadema Kanda ya Ziwa wanapinga Chadema kujiunga na UKAWA huku ikiwata Viongozi wa CHADEMA kuachana na Umoja huo.


Alphonce Mawazo ambae ni Mwenyekiti wa CHADEMA kutoka Mkoani Geita na Mshuda Wilson ambae ni Mwenyekiti wa CHADEMA kutoka Mkoani Simiyu, huku wakiwawakilisha wenzao wa Mikoa ya Mwanza na Kagera, walikanusha taarifa iliyotolewa jana na baadhi ya Vyombo vya Habari ikiwataka Viongozi wa CHADEMA Taifa ambao ni Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu wake Dk.Willbrod Slaa kuachana na Muungano wao wa UKAWA la sivyo watapambana na nguvu ya Wananchi.


“Tunakanusha taarifa iliyotolewa na Fikiri Migiyo kwa vyombo vya habari akisema yeye ni Mwenyekiti wa Makatibu wa Mabaraza Kanda ya Ziwa Magharibi kwa kuwa mtu huyo ni Muongo na si mwanachama wa Chadema wala si kiongozi wa Chadema kwa kuwa cheo hicho hakipo ndani ya Chama, mbaya zaidi haijui hata Katiba ya Chama”.Alisema Mawazo na Kuongeza...


“Hili ni onyo kwa ambao wanatafuta sifa ya kupata umaarufu ama kujitajirisha kupitia Chadema, kwamba sasa hatutakubali tena, tutawapeleka Mahakamani.Kwa bahati mbaya huyu Fikiri Migiyo tunamtafuta amejificha, haonekani aliko lakini tutakapompata tutamfikisha Mahakamani…Ilieleza taarifa ya bwana Mawazo.
Dk.Slaa (Picha kutoka Maktaba)
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Simiyu Mshuda Wilson ameeleza kuwa suala la baadhi ya Watu kuibuka na kusema wao ni viongozi wa Chadema na kuanza kukichafua halitakubalika hivyo Chama hakitavumilia upotoshaji huo.



“Kwanza huyu alietoa taarifa hizi kwa niaba ya Viongozi wa Chadema kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa hajui hata mfumo wa chama kwa kuwa amesema Simiyu iko Kanda ya Ziwa Maghari na Kiutaratibu Simiyu iko Kanda ya Ziwa Mashariki hivyo huo ni Upotoshaji wa Makusudi akijua kabisa nini ambacho anakifanya.Alisema Mshuda.


Aidha aliwasihi wananchi kutoamini kila wanachokisia ama kuandikwa kwa Kuwa UKAWA imeundwa kwa ajili yao kwa lengo la kupigania maoni yao waliyoyasilishwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili iweze kupatikana katiba ya wananchi kupitia maoni yaliyokusanywa kwa gharama kubwa.
Mawazo (Picha kutoka Maktaba).
 Katika magazeti ya Jana ya Mtanzania na Uhuru kulikuwa na Habari zilizodai kwamba Viongozi wa Chadema Taifa wamepewa Siku 14 wawe wamejitoa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vinginevyo nguvu ya Wananchi na ile ya viongozi wa Kanda nyingine itatumika kuwaondoa.Tamko ambalo lilidaiwa kutolewa na Viongozi wa Chadema kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

No comments:

Powered by Blogger.