LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAFUNZI WA CHUO CHA KILIMO SUA MKOANI MOROGORO WAGOMA.

Majengo ya Chuo
Wanafunzi wa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro kitivo cha uhandisi wamegoma kuingia madarasani hii leo ili kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kutafuta njia mbadara ya kuwapatia fedha za kujikimu na chakula pindi wakisubili fedha za mkopo kutoka bodi ya mikopo ambazo zimechelewa kutolewa.

Wakati Mgomo huo Wanafunzi hao wamesema kuwa hali yao ni mbaya na hawezi kusoma kutokana na mazingira waliyonayo kwa sasa kwani hata chakula kukipata kwao imekuwa
ni changamoto kubwa.

Wakati hayo yakijiri Mkoani Morogoro, nako Mkoani Dodoma hali ni tete katika Chuo cha UDOM huku taarifa zikichomoza chini kwa chini kuwa hali kwa wanafunzi wa chuo hicho hususani ni mbaya hatua inayowafanya hadi kujiingiza katika biashara ya ngono katika viwanja wa Ukumbi wa Bunge, huku tatizo la uchelewesha wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu likiwa linazidi kulalamikiwa mara kwa mara hali ambayo inapelekea kuibuka kwa migomo na maandamano ya wanafunzi katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
Karibu Sokoine
Kwa upande wa Wanafunzi wa chuo cha sokoine cha kilimo(SUA) kitivo cha uhandisi wao wameshindwa kuvumilia hali ya ukata inayowakamba na kuamua kugoma kuingia madarasani huku wakisema maisha wanayoishi kwa sasa sio rafiki kwa masomo kutokana na ukosefu wa fedha hizo.

Juhudi za mkuu wa idara ya uhandisi kuwashauri kurejea madarasani ziligonga mwamba baada ya wanafunzi hao kuendelea na msimamo wao ambapo Afisa mikopo wa chuo hicho hakupatikana ili kutolea ufafanuzi jambo hilo kwa madai yuko safarini jijini Dar es salaam huku uongozi wa chuo hicho ukigoma kulizungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari hadi kikao cha ndani kitakapofanyika.

No comments:

Powered by Blogger.