LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA CBE TAWI LA MWANZA KUANZA UJENZI WA MAJENGO YAKE MAPYA.


Wadau wa Elimu ya Biashara wakiwa katika majadiliano ya namna ya ujenzi wa Chuo cha CBE Tawi la Mwanza unavyopaswa kuwa.Wadau hawa walikutana jana katika Ukumbi wa Hotel ya JB Belmont.


Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza kinatarajia kuanza ujenzi wa Majengo yake mapya kuanzia mwezi July mwaka huu, kwa lengo la kupanua wigo wake wa utoaji wa elimu ya biashara hapa nchini.

Mkurugenzi wa Chuo hicho Eustance Joel Mukayu ameyasema hayo hii jana Mkoani Mwanza baada ya kukutana na wadau mbalimbali wa elimu Mkoani Mwanza kwa lengo la kujadili mipango na maelengo yatakayofanikisha ujenzi huo kukamilika kama ilivyokusudiwa.

Mukayu amebainisha kuwa kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaomba kujiunga na elimu ya biashara katika chuo hicho kuwa kubwa, Uongozi wa Chuo hicho umeazimia kupanua wigo wake kwa kujenga majengo yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi zaidi. Tazama picha na Soma maelezo yake pia.
Wadau wa elimu ya Biashara wakiwa katika majadiliano.

Majengo ya Chuo hicho yanatarajiwa kujengwa katika eneo la Kiseke Wilaya ya Ilemela na yatakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi elfu kumi hali ambayo itaongeza idadi ya wanafunzi wanojiunga na chuo hicho kila mwaka, ikilinganishwa na takribani wanafunzi mia tano wanaojiunga na chuo hicho kwa hivi sasa.

Baadi ya wadau wa elimu wameelezea kufurahishwa na hatua ya ujenzi wa chuo hicho kwa kuwa itatoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kujiunga na elimu ya biashara hapa Mkoani Mwanza huku wakiwa na matumaini ya eneo la Kisesa kupata huduma mbalimbali za kimaendeleo kutokana na ujenzi wa chuo hicho katika eneo hilo.
Mapokezi yalikuwa ya hali ya juu.
Eustace Joel Mukayu ambae ni Mkurugenzi wa Chuo cha CBE Tawi la Mwanza.
Kushoto ni Eustance Joel Mukayu ambae ni Mkurugenzi wa Chuo cha CBE Tawi la Mwanza na Kulia ni Paulina David mwandishi wa habari kutoka Radio Free Afrika (RFA).
Kushoto ni Martin Rajab, Afisa Mikopo CRDB Mwanza akitoa maoni yake juu ya ujenzi huo wa Chuo cha CBE Tawi la Mwanza. Ambapo anasema ujenzi wa chuo cha CBE Mwanza utatoa fursa kubwa zaidi kwa wanafunzi kupata elibu bora zaidi juu ya masuala ya biashara.Kulia ni Paulina David Kutoka RFA.
Martin Rajabu ambae ni Meneja Mikopo kutoka Bank ya CRDB Mkoa wa Mwanza.
Fatuma Matope kutoka Ofisi ya Katibu Tawala) Mkoa wa Mwanza ambapo yeye alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza katika majadiliano ya wadau wa elimu ya biashara Mkoani Mwanza.
Dismas Vedastus ambae ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi CBE Tawi la Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.