LIVE STREAM ADS

Header Ads

KILA KITU HIVI SASA NI MAAMUZI. HATA MAPENZI NYUMBANI NI MAAMUZI. ICHEKI HII LIVE MWENYEWE.

Natty E wa kwanza Kushoto akiwa na Oxs Okeleky katikati na pembeni ni msanii Dabo wakati wakizungumzia kampeni ya Mapenzi nyumbani ambayo inatarajiwa kuzinduliwa June 22 mwaka huu Jijini Mkoani Mwanza. Ilikuwa katika kipindi cha Jam Session leo mchana katika Studio za 99.4 Radio Metro. Mapenzi Nyumbani Campainy ni Kampeni rasmi ya kujenga uzalendo wa Kuanza kupenda vitu vya nyumbani kabla ya vile vya nje .Ni Kampeni itakayokuwa na activities nyingi na activity ya kwanza itakuwa FREE STAGE yaani JUKWA HURU. Free Stage ni Makutano ya wasanii wa fani mbalimbali kukutana na kupeana michongo...kuonyesha products zao na ikiwezekana kuziuza pia. Tarehe 22 mwezi huu wa sita Free Stage ya Kwanza itafanyika maeneo ya Kona ya Bwiru maarufu kama Gogo Vivu kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili za jioni. Kumbuka hakuna kiingilio ni BUREEEEEE  yaani Kabang'aaaaa mara DABO huyu hapa sasa...UNA NINI USIPENDE VYA NYUMBANI?

Lulu kutoka Kiss FM (kushoto) akiwa na Bizzo kutoka RFA ndani ya Studio za Metro FM hii leo wakizungumzia kampeni ya Mapenzi nyumbani ambayo imelenga kujenga uzalendo wa kuanza kupenda vitu vya nyumbani kabla ya vile vinavyotoka nje.
Bizzo mtangazaji wa RFA ndani ya Studio za Metro FM jijini Mwanza.
Lulu ambae ni Mtangazaji wa Kiss FM ndani ya 99.4 Metro FM.
Oxs Okeleky msanii na Producer wa Metro FM (kusho), Lulu kutoka Kiss FM na Msanii Dabo wakiwa Metro FM.
Anaanza Oxs, Lulu, Natty E, na Dabo.
Anaanza Lulu, Mwanaharakati George Binagi kutoka Metro FM na Mtanzania Media akifuatiwa na Dabo.
Anaanza Bizzo, Lulu, Oxs na Dabo.SHUKURANI ZA DHATI KWA 99.4 RADIO METRO FM live kutoka Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.