LIVE STREAM ADS

Header Ads

HABARI PICHA: THE SUPER STAR SHOW WIKI HII NDANI YA GOLD CREST HOTEL ILINOGA SANA.

Inafahamika kama The Super Star Show. Ni show kwa maana ya jina lakini ukweli ni kwamba ipo kwa ajili ya mafunzo zaidi. Ni show kwa ajili ya Wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kingereza Maeneo ya Makongoro Kliniki Jijini Mwanza, Maarufu kama English Club ambao kila ijumaa huwa na debate kwa ajili ya kujitanua zaidi katika kuongea kiingereza. Motion Hutolewa na washiriki huwasilisha maoni yao kwa lugha ya kiingereza huku wakiwa wamechangamana na washiri wengine mbalimbali kutoka nje ya English Club lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuongea lugha ya kiingereza mbele ya Umati wa watu. Ijumaa hii The Super Star Show ilifanyika katika Hoet ya Gold Crest kuanzia saa 12 za jioni hadi saa 2 za usiku. Na hawa ni baadhi ya washiriki wakiwa na Mr.English (mwenye shati jeusi).
Huwa ni mwendo wa bata plus kuongea kiingereza huku anaekiuka mashariti ya kuongea kiingereza akitozwa faini.Mbali ya kuwa na Debate, The Super Star Show pia hujumuisha michezo mbalimbali ambapo washiriki hucheza michezo hiyo kwa uhuru huku wakiwa wanaulizana na kujibizana kwa lugha ya kiingereza ambapo mziki kwa yule ambae bado lugha ya kiingereza ni kizaa zaa, huwa ni full kujikanyaga but hatimae hujikuta akiongeza weledi wa kuongea kiingereza kwa mfumo huo. The Super Star Show huwa ni Kila Ijumaa saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana huku nyingine ikiwa ni kuanzia saa 12:00 za jioni hadi saa 2:00 za usiku ambapo watu wote hupewa nafasi ya kushiriki bila kujalisha kama ni mwanafunzi wa English Club ama laaaa! 

No comments:

Powered by Blogger.