LIVE STREAM ADS

Header Ads

SAMAHANI KWA PICHA HIZI: KIKONGWE AUAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA KAHAMA.

Bibi mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina. 


Jinsi Bi Rebeka alivyopigwa shoka kichwani hadi ubongo kutoka nje

Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala kusaidia kuanika Dengu. 

Katika maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na kumkuta Rebeka ameuawa. 

Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo. 

Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwari

Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.

No comments:

Powered by Blogger.