LIVE STREAM ADS

Header Ads

HILI NDILO AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KWA WATENDAJI NA WAKURUGENZI WOTE HAPA NCHINI.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt.Binilith Mahenge (Kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto), Akikagua Mabanda ya maonyesho ya siku ya Mazingira duniani.
Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal amewataka Watendaji na Wakurugenzi wa Halmashauri zote kwa kushirikiana na wadau mbalimba hapa nchini, kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa sera zinazozingatia uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira, ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamebainishwa leo katika taarifa yake iliyosomwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rasi anaeshughulikia Mazingira Dkt.Binilith Mahenge, ambae amemwakilisha katika ufunguzi wa Maadhimishoa ya Siku ya Mazingira duniani ambayo Kitaifa yanaadhimishwa Kitaifa katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza kuanzia June 02 hadi June 05 mwaka huu.

“Tunapoadhimisha siku ya Mazingira duniani, Watendaji na Wakurugenzi wa Halmashauri zetu tukumbuke kusimamia utekelezaji wa mambo yafuatayo; Kampeni ya Kitaifa ya upandaji miti, inayozitaka kila halmashauri kupanda miti isiyopungua milioni 1.5 na kuwasilisha taarifa zao Ofisi ya Makamu wa Rais” Alisema Dkt.Mahenge.




 Amebainisha pia kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa hatua za haraka za kuhifadhi Mazingira ya ardhi na vyanzo vya maji wa mwaka 2006, sanjari na Mkakati wa hatua haraka wa kuhifadhi Bahari, Ukanda wa Pwani, Mito na Mabwawa wa mwaka 2008.

Aidha amesisitiza juu ya Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Februari 12 mwaka 2012, pamoja na Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa Mwaka 2012, utekelezaji ambao kwa pamoja utasaidia kuhifadhi Mazingira kwa kiwango kikubwa.
Huu ndio ushindi wa Jiji la Mwanza, Jiji safi nchini mara nane mfululizo...vipi mwaka huu? tungoje...
Hatimae shughuli ilitamatishwa hivi....Ukifika katika maonyesho hakikisha unafika katika banda hili.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amebainisha kuwa katika kukabiliana na athari za Tabianchi, bado Mkoa wa Mwanza unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na suala la Ukame ambao unaathiri zoezi la uoteshaji wa miche na upandaji wa miti ambapo amezitaja Wilaya za Kwimba, Magu na Misungwi kukumbwa na hali hiyo zaidi.

Pia amezitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na Ukataji wa Miti holela kwa ajili ya Mkaa na Mbao, Uvuvi haramu kwa kutumia sumu, uchimbaji holela wa madini sanjari na uvamizi wa maeneo ya mistu kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na makazi ya watu.

Ambapo amebainisha kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, Mkoa wa Mwanza umechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya Uhifadhi wa mazingira sanjari na kuhamasisha upandaji miti pamoja na kusimamia sheria za nchi ambazo zinahimiza juu ya utunzaji wa mazingira.
                           
Aidha Ndikilo amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa Kushirikiana vyema na Viongozi wa Jiji la Mwanza sanjari na Manispaa ya Ilemela katika kusimamia zoezi la kufanya Usafi wa Mazingira ifikapo jumamosi ya kwanza ya kila mwezi.
Katika Maadhimisho hayo, shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo yote, kuhamasisha wananchi kuhusiana na utunzaji wa mazingira kwa njia ya makongamano.

Shughuli nyinge ni kupanda miti, kuzoa takataka, maonyesho ya utunzaji wa mazingira, kuondoa magugu maji katika ziwa Victoria, ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara katika maeneo yanayojishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimishao hayo, ambapo anatarajiwa kuwakabidhi tuzo washindi mbalimbali wanaoshiriki katika Shughuli za Utunzaji wa Mazingira, ikiwemo Tuzo ya Rais ya Kuhidhadhi vyanzo vya maji, kupanda na kutunza miti. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kitaifa ni “ Tunza Mazingira ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi”.

No comments:

Powered by Blogger.