HOSPITAL YA BUGANDO YAMTIMUA MGONJWA ALIYEOZA MAKALIO, ALIYEBAINI KUWA MAKALIO YAMEOZA AZIRAI, MGONJWA AISHIA KWA MGANGA WA JADI.
Aliyezimia baada ya kuona kidonda |
Mganga wa asili anayemtibu Luhogola |
KASHIFA
nzito imeikumba Hospitali ya rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza baada ya
kudaiwa kumtimua Mgonjwa wake ambaye ameozea Wodini hapo na sasa
anaendelea kuoza akiwa nyumbani kwa mganga wa tiba za asili.
Aliyetimuliwa
Hospitalini hapo ni Joseph Luhogola (38),mkazi wa Kitongoji cha
Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita.
Luhogola
alipokelewa Hospitalini hapo Apr 22 mwaka huu akitokea katika Hospitali
ya Wilaya ya Chato ikiwa ni saa chache baada ya kupata ajali.
Ajali
hiyo ilitokea Apr 22 katika Kijiji cha Lubambagwe Wilayani Chato,ambapo
gari aliyokuwa ameipanda Luhogola aina ya Hiace akitokea Geita kwenda
Mganza ilipofika eneo hilo na kupinduka baada ya kuchomoka gurudumu la
mbele na baadaye la nyuma.
Kufuatia
ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7 mchana,Luhogola huku akiwa
amepoteza fahamu alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato ambako
hata hivyo alipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuchukuliwa na gari la
Hospitali hiyo hadi Bugando.
Kwenye
Hospitali ya Rufaa ya Bugando alipokelewa na kulazwa wodi E namba 803
ambayo ni ya wanaume iliyoko katika ghorofa la 8 kwenye majengo ya
Hospitali hiyo.
Hata
hivyo imeelezwa kuwa,baada ya madaktari kuchunguza afya yake ilibainika
kuwa alikuwa na tatizo la uti wa mgongo na alishauriwa kulala chali
muda wote kama tiba ya tatizo alilokuwa nalo.
Wakati
wote akiwa Wodini hapo,mke wake Keflini Kafaransa(36) alikuwa akizuiwa
kukaa wodini kwa mumewe kwa alichoelezwa sheria za Hospitali hiyo
haziruhusu mwanamke kukaa kwenye wodi ya wanaume kwa muda mrefu.
Kutokana
na hali hiyo,Kafaransa alilazimika kumtafuta shemeji yake Hatari
Petro(21)ambaye ni mdogo wa Luhogola na ndiye aliyechukua jukumu la
kumuuguza kaka yake huyo kuanzia Apr 28 hadi anatimliwa kwenye hospitali
hiyo.
Akisimulia
mkasa huo,Luhogola ambaye kwa sasa yu mahututi nyumbani kwa mganga wa
tiba za asili za mifupa katika Kitongoji cha Elimu,Kijiji cha Nyankumbu
Wilayani Geita alisema hakutegemea kama Hospitali kubwa kama Bugando
ingeweza kumuaga akiwa katika hali hiyo.
Luhogola
ambaye kwa sasa amepooza kuanzia kifuani hadi miguuni anadai kuwa,iwapo
angejua hayo yangetokea angewashauri ndugu zake wasimpeleke kwenye
Hospitali hiyo kwa kuwa tatizo alilonalo la kuoza makalio yake
lilisababishwa na wauguzi waliokuwa wakimhudumia.
CHANZO CHA AJALI YAKE
Akifafanua
ajali ilivyotokea,Luhogola alisema ‘’Nakumbuka nilikuwa mbele kwa
dereva ,gari ilibasti tairi ya nyuma na baadaye ya mbele ilikuwa mwendo
kasi na kuhama barabarani,gar iliviringika na mimi nikiwa mbele
nilipitia kioo cha mbele cha dereva nilikuwa natoka Geita na sikujua
tena kilichoendelea hapo maana nilipoteza fahamu na nilipoijiwa na
fahamu nilikuwa Bugando na nikagundua nimeumia kichwani na kifuani’’
AKIWA BUGANDO
‘’Nakumbuka
nilipopata fahamu nikiwa Bugando,niligundua nina majeraha madogo madogo
sehemu za kichwani ambayo hata hivyo hayakuchukua muda na yalipona kwa
muda mfupi lakini niliendelea kukaa wodini hapo baada ya madaktari
kunieleza ninatatizo la uti wa mgongo’’
‘’Nilipowauliza
tiba za ugonjwa huo daktari aliyekuwa anakuja kunitizama wodini hapo
alinieleza kuwa,hakuna tiba ya ugonjwa huo zaidi ya kulala chali bila
kugeuzwa geuzwa name nikakubali’’
‘’Hata
hivyo nikiwa wodini hapo nilipooza mwili kuanzia kifuani hadi miguuni
hivyo nikapoteza mawasiliano kutoka sehemu ya mwili ulioopooza hadi
miguuni’’
Alidai
kuwa,kutokana na kupooza kwake hakuweza kujua kinachoendelea na alikuwa
akiona manesi wakimfuata alipolala kisha kumgeuza kifudifudi na baadaye
kumlaza chali kama maelekezo ya daktari aliyedai hiyo ndiyo tiba ya uti
wa mgongo.
Alidai
kuwa,siku moja baada ya manesi kumlaza kifudifudi kwa muda mrefu na
baadaye kumlaza tena chali aliamua kuhoji na ndipo alipoelezwa
anakijiupele kidogo sehemu za makalio‘’
‘’Ilikuwa
kama ada ya manesi kufika na kunigeuza nalalia tumbo(kifudifudi)bila
kujua walichokuwa wanakifanya maana kutokana na kupooza kwangu sikuhisi
maumivu yoyote’’
‘’Hata
hivyo mtindo huo uliendelea siku baada ya siku na ndipo siku moja
nilipoamua kuhoji kulikoni baada ya kunilaza kifudifudi kwa muda mrefu
na ndipo waliponiambia nina upele kwenye makalio hivyo walikuwa
wananisafisha’’alisema Luhogola kwa sauti isiyo na matumaini.
Kutokana
na majibu hayo ya manesi,Luhogola alidai kuwa manesi hao waliendelea na
utaratibu huo hadi alipoagwa Hospitalini hapo akiambiwa amepata nafuu
bila kujua makalio yake yalikwisha oza hadi kwenye uti wa mgongo huku
ndani ya kidonda kukijazwa bandeji kumwezesha kukaa.
‘’Mimi
nahisi Madaktari walikuwa hawajui kama nina kidonda na manesi ndio
waliwaficha madaktari,maana manesi walikuwa wananigeuza na kunisafisha
na kunirudisha hivyohivyo’’
‘’Nikiwauliza
manesi mbona wananisafisha muda murefu wanadai hakuna kitu maana sina
hisia za maumivu yoyote’’alisema kwa sauti ya kukwaruza
MKEWE AZUNGUMZA
Akizungumza
na JAMHURI mke wa Luhogola,Kefline Kafaransa(36)alidai kuwa muda wote
waliokuwa wodini hapo hakuweza kubaini janja nyani ya manesi waliokuwa
wakimhudumia mumewe ya kujaza bandeji sehemu ya makalio kilipo kidonda
hicho.
Kafaransa
anataja sababu za kutogundua iwapo mumewe alikuwa na kidonda kikubwa
kwenye makalio ambacho kilijazwa mabandeji na manesi hao kwa kuwa muda
wote alipokuwa akiingia wodini hapo alifukuzwa na wauguzi hao.
‘’Yaani
ile wodi nilipokuwa naingia kumjulia khali mume wangu,manesi
walinifukuza hivyo sikuweza hata kubaini kama mume wangu anakidonda
kikubwa kiasi kile na siku zote niliambiwa ile ni wodi ya wanaume mimi
kama mwanamke sipaswi kukaa mle kwa muda mrefu’’
Kufuatia
hali hiyo Kafaransa anadai kuwa,hakuona huduma yoyote aliyokuwa
akifanyiwa mumewe huyo zaidi ya kumkuta akiwa amelala chali muda wote.
Kwa
mjibu wa Kafaransa,mbali na madaktari kumweleza mumewe angelikaa wodini
hapo kwa muda wa wiki 6 akipatiwa huduma ya tiba za uti wa mgongo
alishangaa kuona wakiagwa Mei 27 kabla ya muda huo huku wakitozwa
gharama kubwa tofauti na huduma yenyewe.
‘’Madaktari
baada ya kutupokea na kugundua tatizo la mume wangu walidai kuwa tiba
ya mtu mwenye tatizo hilo lazima akae wodini kwa muda wa wiki 6 lakini
nilishangaa kuona tunaagwa kabla ya muda huo huku gharama tulizotozwa
zikiwa ni kubwa.
‘’Wakati
tulikwishaambiwa tutakaa pale na mgonjwa wetu kwa wiki 6,nilishangaa
Tarehe 26 baada ya daktari kupita mzunguko 27/05/2014 saa 6 tuliagwa
rasmi kwa kulipa madeni yote tuliyokuwa tunadaiwa kiasi cha Tshs
119,000.00 kama malipo ya huduma tuliyoipata hospitalini hapo pesa
ambayo ni kubwa na nadhani tulitozwa ili kununua kidonda alichokipata
akiwa wodini hapo.
MDOGO WAKE ANENA
Kwa
upande wake,Hatari Peter(21)ambaye ndiye alikuwa akiingia wodini hapo
mara kwa mara kumjulia hali kaka yake huyo alidai kuwa hata yeye
hakuweza kubaini iwapo kaka yake ameoza sehemu za makalio kwa kile
alichodai muda wote alimkuta amefunikwa shuka la Hospitali hiyo.
Peter
ambaye alikuwepo wodini hapo wakati wakiagwa,alidai kuwa huku akijua
kaka yake amepata nafuu kwa mjibu wa daktari aliyemuaga,walielezwa kuwa
watafute gari ya kukodi ili wamlaze kaka yake juu ya godoro hadi
nyumbani.
Daktari
aliyewaaga aliwaambia hata wakifika nyumbani waendelee kumlaza chali
mgonjwa wao hadi hapo mgongo utakapotengemaa vizuri huku wakionywa
kutomfanyisha kazi ngumu.
‘’Yaani
yale maneno matamu aliyokuwa akitueleza Yule daktari kwa mtu yeyote
angehisi kuwa mgonjwa wetu ameshapona kabisa kumbe walikuwa wametuingiza
mjini kwani kama tungejua kaka hana makalio na anakalia bandeji
tusingekubali kumtoa hapo wodini na kama noma basi ingekuwa
noma’’alisema na kuongeza
‘’Yule
daktari kwa kinywa chake alitutamkia kwamba hali ya kaka kwa muda huo
ilikuwa imetengemaa kabisa tena akamwambia na kaka kwa kumhusia ‘’Joseph
uende nyumbani ,wakukodishie Gari wakubebe waweke godoro na ukifika
nyumbani uendelee kulala mpaka mwezi wa nane ‘’alisema Peter akinukuu
maneno ya Yule Daktari na kuongeza
‘’Akamuuliza
tena kaka ‘’Joseph unafanya kazi gani,alipojibiwa ni mfanyabiashara wa
dagaa daktari Yule aliongeza ‘’Hiyo biashara huiwezi na kama ndugu yako
ana uwezo wakununulie baiskeli ya miguu mitatu na wakufungulie biashara
ya kibanda uwe unauza sawa Joseph”alisikika akimhusia mgonjwa wao baada
ya kuagwa hospitalini hapo.
Kwa
mjibu wa Peter,walifanya kama walivyoelekezwa kwa kukodi gari kisha
kumlaza kwenye godoro hadi nyumbani kwa kaka yaom aishie mjini Geita
ambako ndiko walipogundua kuwa makalio yake yameoza huku kukiwa
kumejazwa bandeji ndani yake.
ALIYEMPOKEA APOTEZA FAHAMU BAADA YA KUGUNDUA KIDONDA
Msitapher
Luhogola(40) ambaye ni kaka wa mgonjwa huyo aliyepooza na kukosa
matumaini huku akitibiwa kwa tiba za jadi anadai kuwa yeye ndiye
aliyegundua kidonda hicho muda mfupi baada ya kumpokea akitokea Bugando
hali iliyopelekea kupoteza fahamu kutokana na mshituko alioupata baada
ya kuona kidonda hicho.
Msitapher
alifafanua kuwa,baada ya kumpokea mdogo wake huyo,ambaye alikuwa
amevalia nguo zake nzuri aligundua harufu Fulani wakati akimshusha
kwenye gari iliyomtoa Bugando akimuingiza ndani ya nyumba yake na kuamua
kuchunguza kwa makini harufu ilikokuwa ikitokea kwenye mwili wa ndugu
yake huyo.
‘’Baada
ya kumfikisha nyumbani ndio niligundua anatoa harafu ikabidi nimlaze
kitandani na kuanza kumkagua na ndipo nikagundua alikuwa amezungushiwa
bandeji sehemu ya makalio yake nikachukua jukumu la kumfungua bandeji
zile ili kuona na ikibidi nimsafishe’’
‘’Ndugu
yangu,nilijikuta napiga kelele kama mtu aliyeona mnyama mkali kwani
sikuamini kama ningekuta ndugu yangu hana makalio yalishaoza maana
nilikuta kwenye makalio amerundikiwa mabandeji lundo yamesondekwa kilipo
kidonda’’.
Msitapher ambaye alimpokea ndugu yake huyo majira ya jioni ya Mei 27 anadai
kuwa, baada ya kufungua kisha kutoa yale mabandeji yaliyokuwa
yamesondekwa ndani ya kidonda hicho alijikuta akipoteza fahamu na
kuwalazimu ndugu na jamaa waliokuwa wamekusanyika chumbani humo kufuatia
kelele alizopiga kuanza kumpepea na alizinduka baadaye huku asijue la
kufanya.
‘’Baada
ya kurejewa na fahamu ndiyo nikaanza kukiosha na mpaka sasa naendelea
kukiosha na tupo kwa mganga huyu wa jadi ambaye anamtibu kwa tiba
za kienyeji kwa maana dawa za kizungu zimeshindikana’’
‘’Kama
wamemfukuza hospitali,sisi kama ndugu tumetafuta mbadala mwingine
kuhakikisha tunaokoa maisha ya mwenzetu’’alisema kwa uchungu na kuongeza
‘’Sikuamini
kama hospitali kama Bugando ambayo ni ya rufaa kama inaweza kufikia
hatua ya mgonjwa kuoza wakati kuna wataalamu wa kutosha na wakamuaga mtu
mwenye kidonda kama hicho,kwa hiyo orodha ya pesa tuliyolipa tulikuwa
tunanunua kidonda ambacho kimesababishwa na hospitali hiyo’’
‘’Au
tunachangia hiyo pesa jengo la Bugando liendelee kuwepo kama Bugando au
pesa hiyo ni kwa manufaa ya madaktari na wauguzi mpaka sasa
sielewi,kama kuna msaada zaidi juu ya matibabu hasa kama haya ambayo
wamesababisha wenyewe kwa mgonjwa basi Serikali iingilie kati hasa
waziri wa afya ili ndugu yangu asaidiwe’’alisema kwa masikitiko.
NYARAKA ZA HOSPITALINI HAPO
Jamhuri
limebahatika kuona nyaraka mbalimbali ambazo zinadhihirisha
kwamba,mgonjwa huyo amewahi kulazwa katika hospitali hiyo kabla ya
kuagwa.
Nyaraka
hizo pamoja na mambo mengine zinaonyesha kiasi cha pesa walizolipa
Hospitalini hapo,baadhi ya madaktari na wauguzi waliompokea na
kumhudumia,na namba 973807 ambayo ndiyo ulikuwa usajili wa mgonjwa huyo
kuingilia kwenye Hospitali hiyo.
Baadhi
yao ni Dokta Ernest Etuonguo aliyempokea Apr 22,Dokta G. Daniel
aliyechunguza afya yake,pamoja na Dokta Shanel aliyemuaga Mei 27,huku
muuguzi aliyefahamika kwa jina la Mage akidaiwa ndiye aliyekuwa wodini
hapo akitoa huduma mbalimbali ikikwemo dawa kwa mgonjwa.
MTOA TIBA ZA JADI ATOA YA MOYONI
Kwa
upande wake Paul Chasama ambaye ni mtaalamu wa tiba za jadi kwa kuunga
mifupa na kurudisha viungo vya mwili vilivyochengana ambaye ni mkazi wa
Kitongoji cha Elimu,katika kijiji cha Nyankumbu Wilayani Geita amedai
kuwa,kutokana na uzoefu kwenye kazi hiyo anao uhakika wa asilimia mia
kwamba Luhogola atapona.
Chasama
aliyedai kurithishwa ujuzi huo na marehemu baba yake mzee Chasama
Luswigilo alidai kuwa,kutokana na uzoefu wake wa miaka mingi kwenye kazi
hiyo ndugu wa mgonjwa waendelee kumwamini kama walivyomwamini
kumkabidhi mgonjwa wao na kwamba si muda mrefu atarejea katika hali yake
ya kawaida.
Akifafanua
kauli yake,Chasama alidai kuwa,amekwishakutana na wagonjwa wengi wenye
matatizo makubwa tofauti na alilonalo Luhogola na walipona na kurejea
katika afya zao na kwamba kwa uzoefu wake katika kipindi cha mwezi mmoja
mbele atakuwa amepona.
‘’Mimi
ndiye Chasama kama umewahi kumsikia ninachokueleza ndugu mwandishi huyu
mgonjwa katika kipindi cha mwezi mmoja mbele atakuwa anadunda mtaani
kwa hili tatizo la kupooza kwake,na kuvunjika uti wa mgongo na hata hiki
kidonda ndani ya wiki tatu kitakuwa kimepona maana nimeshaanza kuweka
dawa ya kuotesha nyama’’alitamba Chasama
Akielezea
chanzo cha wagonjwa wa kupooza,alidai kuwa hutokana na mshituko ambao
husababisha mipira iliyo ndani ya mgongo kukatika na kupoteza
mawasilianao ya mwili.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo Jijiji Mwanza Profesa Charlesr
Majinge alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya kiganjani namba
0754-454724 ili kuzungumzia sakata hilo hakupatikana na hata
alipopatikana simu yake ilionyesha imepokelewa na baadaye ilizima.
Jamhuri
halikuchoka liliamua kumwandikia ujumbe wa maandishi kuuliza iwapo
wataalamu wa hospitali hiyo walishindwa kutibu kidonda hicho na badala
yake kuamua kukificha kwa kukijaza bandeji hadi kilipogunduliwa na ndugu
zake baada ya kufikishwa nyumbani kwako,hata hivyo hakujibu. Hata hivyo
Jamhuri litaendelea kumtafuta na litawajuza wasomaji wake hatua kwa
hatua juu ya sakata hili.
Kwa hisani ya Mitandao ya Kijamii.
Kwa hisani ya Mitandao ya Kijamii.
No comments: