LIVE STREAM ADS

Header Ads

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA TAARIFA KUHUSIANA NA WATU WALIONG'ANG'ANIA KATIKA MWILI WA ALBINO BAADA YA MAUAJI MJINI NANSIO.



Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limekanusha taarifa ya kutokea kwa mauaji ya Mtu mmoja ambae ni Mlemavu wa ngozi katika Mji wa Nansio Wilaya ya Ukerewe huku watu waliotekeleza mauaji hayo wakidaiwa kung’ang’ania katika mwili wa marehemu huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza SACP.Valentino Mlowola ametoa taarifa hiyo hii leo wakati akizungumza na Radio Metro kuhusiana na tukio hilo, ambapo amebainisha kwamba taarifa za kutokea kwa mauaji hayo zilianza kusamba tangu juzi Katika Mji huo wa Nansio na hivyo kusababisha taharuki kubwa kwa wananchi wa Mji huo.

Amesema kuwa baada ya taarifa hizo kuenea Mjini Nansio, wananchi wengi waliweza kujikusanya na kwenda katika Mochwali ya hospitali ya mji huo wa Nansio kwa ajili ya kutaka kushuhudia mwili wa mtu alieuawa maada ya taarifa kusambazwa kuwa watu waliotekeleza mauaji hayo walikuwa bado wameng’ang’ania katika mwili wa marehemu huyo.

Kamanda Mlowola amebainisha kwamba baada ya taarifa hizo kuenezwa katika mji huo wa Ukerewe wananchi wengi walikusanyika katika Mochwali ya Hospitali ya Mji wa Nansio ili kushuhudia tukio hilo hali ambayo iliwalazimu polisi kutumia nguvu ili kuweza kuwatawanya.

“Kwanza naomba kusema kuwa tukio la kuuawa alibino na watu kugandana halikuwahi kutokea, halikuwahi kuwepo.Ni uvumi ulisababishwa na watu ambao hatujui sababu zilizosababisha wasambaze uvumi huo na kutokana na uvumi huo Mji wa Ukerewe majuzi ulikumbana na tafaruku, watu wengi walikwenda mochwari ili kuwashuhudia watua mbao hawapo hivyo ikabidi tutumie nguvu kuwatawanya kwa hiyo naomba kuwambia wananchi kwamba huo ni uvumi ambao hauna msingi wowote na tukio kama hilo halikuwahi kuwepo”.Alisema Kamanda Mlowola.

Kamanda Mlowola ameongeza kuwa jeshi la polisi halina sababu ya kuwadanganya wananchi juu ya tukio hilo ama tukio la aina yoyote hivyo wasiwe wanaamini matukio kama hayo kabla mamlaka husika haijatoa taarifa kamili huku akibainisha kuwa hakuna chanzo cha uvumi huo kwa kuwa uvumi huwa hauna chanzo maalumu hivyo hata siku hiyo katika Mochwari hiyo ya Nansio hakukuwa na mwili wa alibino aliedaiwa kuuawa.

HII NI TAARIFA AMBAYO MTANZANIA MEDIA ILIIPATA HAPO AWALI.

Mlemavu mmoja wa ngozi (Albino) ameuawa Mkoani Mwanza na mwili wake kunyofolewa viungo vyake vya siri huku wauaji waliotenda unyama huo waking'ang'ania katika mwili wa marehemu huyo mara baada ya mauaji hayo.

Tukio hilo limetokea jana katika Mji wa Nansio Wilaya ya Ukerewe ambapo baada ya wauaji kumuua albino huyo na kumkata via vyake vya uzazi walijikuta wakishindwa kuondoka navyo na kung'ang'ania katika mwili wa marehemu huyo.

Mara baada ya mauaji hayo, wananchi wenye hasira walifika katika eneo la tukio na kuanza kuwapiga wauaji hao lakini polisi waliwahi kufika na kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na kufanikiwa kuwaokoa wauaji hao ambao nao nusra wauawe na wananchi.

Baada ya mauaji hayo mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji wa Nansio Wilayani Ukerewe huku wauaji hao wakiwa bado wameng'ang'ania katika mwili wa mlemavu huyo (Albino) alieuawa.

No comments:

Powered by Blogger.