LIVE STREAM ADS

Header Ads

MLEMAVU WA NGOZI AUAWA MKOANI MWANZA, WAUAJI WANG'ANG'ANIA KATIKA MWILI WAKE.

Zuia Ukatili wa aina yoyote katika jamii yako (Picha haihusiani na tukio).
Mlemavu mmoja wa ngozi (Albino) ameuawa Mkoani Mwanza na mwili wake kunyofolewa viungo vyake vya siri huku wauaji waliotenda unyama huo waking'ang'ania katika mwili wa marehemu huyo mara baada ya mauaji hayo.

Tukio hilo limetokea jana katika Mji wa Nansio Wilaya ya Ukerewe ambapo baada ya wauaji kumuua albino huyo na kumkata via vyake vya uzazi walijikuta wakishindwa kuondoka navyo na kung'ang'ania katika mwili wa marehemu huyo.

Mara baada ya mauaji hayo, wananchi wenye hasira walifika katika eneo la tukio na kuanza kuwapiga wauaji hao lakini polisi waliwahi kufika na kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na kufanikiwa kuwaokoa wauaji hao ambao nao nusra wauawe na wananchi.

Baada ya mauaji hayo mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji wa Nansio Wilayani Ukerewe huku wauaji hao wakiwa bado wameng'ang'ania katika mwili wa mlemavu huyo (Albino) alieuawa.
Mtanzania Media: Utapata taarifa zaidi juu ya tukio hili kadri zitakavyopatikana ambapo juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi bado zinaendelea, Zuia Ukatili katika jamii yako.
Zuia Ukatili wa aina yoyote katika jamii yako (Picha haihusiani na tukio).

No comments:

Powered by Blogger.