VITENDO VYA UKATILI DHINI YA WATOTO INCHINI TANZANIA NI TATIZO KUBWA. SHIRIKA LA KIVULINI LAIASA JAMII KUCHUKUA HATUA ILI KUVITOKOMEZA VITENDO HIVYO.
![]() |
Hadija Liganga kutoka KIVULINI. |
Vitendo vya
Ukatili ambavyo wamekuwa wakitendewa watoto wadogo miongoni mwa wanajamii, vimetajwa
kuwa chanzo kikubwa kinachokwamisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto ambao
wamekuwa wakikumbwa na ukatili wa aina mbalimbali hapa nchini.
Hayo yameelezwa jana na Hadija Liganga ambae ni Afisa Sera na Mtandao
kutoka shirika la Kutetea haki za Wanawake na Watoto KIVULINI katika Mdahalo wa
Wadau wa Elimu Jijini Mwanza uliofanyika Katika Hotel ya JB Belmont ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo iliyoadhimishwa jana.
![]() |
Hadija Liganga |
Liganga ambae aliwasilisha Mada ya Vitendo vya Ukatili na Elimu bora, amebainisha
kwamba vitendo vya ukatili dhini ya watoto nchini Tanzania ni tatizo kubwa,
kutokana na namna ambavyo vitendo hivyo vimekuwa vikirudisha nyuma maendeleo ya
watoto ambao wamekuwa wakinyanyswa katika jamii.
Amevitaja miongoni mwa vitendo hivyo vya ukatili kuwa ni pamoja na
ukatili wa Kingono, Kisaikolojia, kimwili, kihisia na hata kimwili huku
akibainisha kuwa jambo la kusikitisha ni kwamba vitendo hivyo vimekuwa
vikitekelezwa na wanajamii wenyewe.
![]() |
Bi Angelina Benedicto kutoka Shirika la WOTE SAWA akiwasilisha mada juu ya Utumikishi wa watoto na Upatikanaji wa Elimu Bora. |
Aidha amebainisha kuwa maeneo mengi hivi sasa katika jamii si salama
kwa watoto kutokana na vitendo vya ukatili kuwasibu watoto katika maeneo hayo,
huku wanajamii wakishindwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa vitendo
hivyo vinatokomezwa kabisa.
Pamoja na changamoto nyingine katika jamii, Liganga ameitaja
changamoto ya Maelewano mabaya miongoni mwa wanajamii kuwa ni mojawapo ya
sababu ambayo imekuwa ikisababisha watoto wengi kukumbwa na vitendo vya
kikatili katika jamii.
![]() |
Jimmy Luhende ambae ni Mkurugenzi kutoka Taasisi ya ADGL akiwasilisha mada ya Utawala bora katika Shule katika mdahalo huo. |
Ili kuwanusuru watoto dhini ya Ukatili hapa nchini, Liganga ametoa rai
kwa wanajamii kila mmoja kwa nafasi kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto katika jamii vinatokomezwa kwa kuamini kuwa mtoto
wa mwenzio ni mtoto wako pia.
![]() |
Wadau wa Elimu |
Shirika la Kutetea Haki za
Wanawake na Wasichana KIVULINI kwa kushirikiana na Wadau wengine liliweza
kuandaa Mdahalo huo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
ambapo mwaka huu Kaulimbiu ilikuwa inasema kuwa Upatikanaji wa Elimu Bora na
Isiyo na Vikwazo ni Haki ya Kila Mtoto.
No comments: