MAHAKAMA YAWAHUKUMU WAPINZANI HUKUMU YA KIFO.
Wanachama wa kundi la Muslim Brotherhood wakiwa kizuizini.
Mahakama moja nchini Misri
imewahukumu vifo viongozi kumi wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim
Brotherhood kwa kuchochea ghasia zilizosababisha vifo vya watu wawili
mwezi July mwaka uliopita.
Raia hao walipatikana na hatia ya kuchochea uma na kuzuia msafara wa magari katika mji wa Qalyub kazkazini mwa mji wa Cairo.
Pia wamedaiwa kuwa wamekuwa wakishiriki katika maandamano dhidi ya jeshi ambalo lilimpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi. Bwana Badie tayari amehukumiwa kunyongwa katika kesi nyengine.
Na:bbcswahili
No comments: