MAKALA: UTAFITI WAGUNDUA KWANINI BODABODA HAWAOGOPI KIFO.
Kwa kweli imelazimika kufanya utafiti wa haraka haraka
kuhusu hii ishu ya hawa jamaa zetu
waendesha Bodaboda. Najua utafiti huu utaingizwa kwenye vitabu vya
kumbukumbu za watafiti bora duniani bila wasiwasi. Utafiti ulilenga
katika kutaka kujua kwanini waendesha Bodaboda hawaogopi kufa wala kuumia.
Baada ya utafiti uliochukua wiki kadhaa sasa kwa mara ya kwanza unawekwa hadharani katika makala hii inayosomwa na watu wengi duniani. Tuligundua kuwa kimsingi waendesha Bodaboda huzaliwa kama binadamu wengine na hukua katika mazingira ya kawaida kabisa, hivyo ubongo wao na wetu sisi raia wengine hauna tofauti kabisa.

Baada ya mchanganuo wa mambo kadhaa
nimegundua kuwa huwa kunatokea mabadiliko makubwa katika mfumo wa ubongo
wa mwendesha Bodaboda mara tu
makalio yake yanapogusa kiti cha pikipiki yake.
Kitendo cha makalio kugusa kiti cha bodaboda kusababisha neva za makalio zipeleke taarifa kwenda sehemu ya ubongo inayoitwa Medula Oblongata, na hapa hutokea mchakatuo wa taarifa za kineva ambazo hupeleka taarifa katika ubongo wa kushoto ambazo huzima sehemu ya ubongo inayohusika na ustaarabu na woga, sehemu hii kitaalamu nimeiita Bongoliasis.
Kuzimwa kwa Bongoloiasis husababisha mwendesha Bodaboda kuamini kuwa pikipiki ina miguu minne na ni nyembamba kama nyoka, hivyo basi haianguki na inaweza kupenya popote bila tatizo, pia inaweza kupaa. Ikianguka hakuna kuumia, ukiumia hapaumi wala hapatoki damu, pakitoka damu ni kidogo tu.
Utafiti umegundua pia pasenja wa Bodaboda hupatwa na athari hizi pia kwa hiyo nao huwa hawalalamiki dereva wao anapoonekana na ulimwengu wote kuwa anachezea kifo.
Athari hizi huacha mara ukiondoka kwenye kiti cha Bodaboda.
Utafiti unaendelea kuona ni dawa gani itumike kuzuia madhara haya, labda
igunduliwe dawa ya kupaka aidha kwenye kiti chenyewe au kwenye makalio ya hawa
jamaa ili kuzuia athari zilizotajwa hapo juu. Na je taasisi gani ipewe jukumu
la kuwapaka hawa jamaa dawa kila asubuhi kabla hawajapanda Bodaboda .Kitendo cha makalio kugusa kiti cha bodaboda kusababisha neva za makalio zipeleke taarifa kwenda sehemu ya ubongo inayoitwa Medula Oblongata, na hapa hutokea mchakatuo wa taarifa za kineva ambazo hupeleka taarifa katika ubongo wa kushoto ambazo huzima sehemu ya ubongo inayohusika na ustaarabu na woga, sehemu hii kitaalamu nimeiita Bongoliasis.

No comments: