MAKAMU WA RAIS ATOA PONGEZI ZAKE KWA COCACOLA JIJINI MWANZA. AWAASA NA WENGINE KUIGA MAZURI HAYA KUTOKA COCACOLA.
Katika kuadhimisha siku ya Mazingira duniani iliyoadhimishwa kesho, huku Kitaifa maadhimisho hayo yakifanyika katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal amekipongeza Kiwanda cha Nyanza Bottling Company ambacho kinazalisha vinywaji jamii ya Cocacola kwa kuzingatia Uzalishaji usiohatarisha Uhifadhi wa Mazingira.
Dkt.Bilal aliyasema hayo alipotembelea kiwanda hicho ili kujionea namza shughuli za uzalishaji zinavyofanyika katika kiwanda hicho.Baada ya kujionea namna kiwanda hicho kilivyo rafiki wa mazingira, alivitaka viwanda na wazalishaji wengine kuiga mfano wa Nyanza Bottling Company katika kuzingatia uzalishaji usioathiri mazingira.

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Kiwada cha
Cocacola, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya
kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani
Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.



Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na
Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa
kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi na kutumika
upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani,
kuoshea magari na n.k.
No comments: