LIVE STREAM ADS

Header Ads

SAGENGO NA RWEKAKA WAKIWA KATIKA STUDIO ZA RADIO METRO MKOANI MWANZA HII LEO.

Emmanuel Sagengo (kulia) na Saad Rwekaka ambao wanatoka katika kamati ya maandalizi ya Siku ya Mtoto wa Afrika Wilaya ya Ilemela wakiwa katika kipindi cha Pambazuko la Metro leo asubuhi wakielezea namna maadhimisho hayo yatakavyofanyika kwa upande wa Wilaya ya Ilemela.Kwa mbali ni Dk.Tonny, Mtangazaji wa kipindi hiki.
Katika Wilaya ya Ilemela Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yatafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, huku katika Wilaya ya Nyamagana yakifanyika katika Uwanja wa shule ya Msingi Buhongwa na Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza yakifanyika katika Wilaya ya Magu.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu ni " Kupata Elimu Bora na Isiyo na Vikwazo ni Haki ya Kila Mtoto.Bonyeza sehemu iliyoandikwa Makala ili kuelewa zaidi juu ya maadhimisho haya.
Saad Rwekaka ambae ni Mjumbe katika kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kutoka Wilaya ya Ilemela.
Emmanuel Sagenge ambae ni Katibu katika Kamati ya Ulinzi na Usalama kutoka Wilaya ya Ilemela ambayo inasimamia Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika hii leo.
Aliphonce Tonny Kapela akiwa katika kipindi cha Pambazuko la Metro kupitia 99.4 Radio Metro FM kinachokwenda hewani kuanzia saa 06:00 hadi saa 09:00 za asubuhi.Watangazaji wengine wa kipindi hiki ni Delphina Kyaruzi na Jacob Jambele Usungu (Hawapo Pichani).

No comments:

Powered by Blogger.