RAIA WA SOMALIA WAKUBALIWA KUWA RAIA WA TANZANIA.
Watoto hawa walikuwa miongoni mwa wale waliopokea vyeti vyao
Serikali ya Tanzania imetoa
vyeti vya uraia wa Tanzania kwa raia wa Somalia zaidi ya elfu moja na
mia tano,ambao kiasili walitokea nchini Tanzania zaidi ya karne tatu
zilizopita.
Raia wa Somalia zaidi ya elfu moja na mia tano walitokea nchini Tanzania zaidi ya karne tatu zilizopita.
Raia hao wapya wa Tanzania wamepewa uraia ikiwa ni kwa mujibu wa sheria za Tanzania baada ya serikali ya Tanzania kuwafanyia usajili na kuridhika kuwa hapakuwa na sababu za kuwanyima uraia huku pia kukiwa na kundi jingine la wasomali wabantu 150 ambao bado wanasita kuomba uraia wa Tanzania.
Naye waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Bwana Mathias Chikawe baada ya kuwakabidhi vyeti vya uraia raia hao aliwataka kujisikia kuwa huru.
Hata hivyo aliwataka kuheshimu sheria za nchi na kutowaruhusu maadui wa nchi kuvuruga amani kwenye kijiji hicho cha Chogo,huku akiwataka kujilinda na matendo ya kigaidi na kutoruhusu kushawishiwa na maadui wanaoweza kutumia njia mbali mbali kama mihadhara ya kidini au kisiasa.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la umoja wa mataifa nchini Tanzania Bi Joyce Mends Cole anasema jukumu lao kwa raia hao sasa limekamilika baada ya kupata uraia,huku shirika hilo likiwa limewajengea zahanati katika kijiji cha Chogo,shule na kuimarisha mradi wa maji ya kunywa.
Vyeti walivyokabidhiwa raia hao
Wengi wanatumia Kiswahili ambacho ni lugha ya asili ya Tanzania lakini pia raia hao wanazungumza kwa ufasaha lugha ya kizigua na sasa wakiwa wameongezea lugha ya kisomali waliyojifunza ughaibuni nchini Somalia.
Inaaminika kuwa nchini Somalia bado kuna Watanzania wengi asilia wanaoishi nchini humo ambao hawana namna wanayoweza kuja nchini Tanzania ingawa wana hamu ya kufanya hivyo.
Na:bbcswahili
No comments: