LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA UMMA: MTOTO ANATAFUTWA.


Mama wa Mtoto huyo.
Mtoto (Kijana) Nyegana Kacha kwa jina la nyumbani (Boniphace Marwa kwa jina la Shuleni) mwenye umri wa miaka 18 Kabila Mungulimi na Raia wa Tanzania Kutoka Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara anatafutwa baada ya kupotea ghafla.

Siku ya Tarehe 04 mwezi wa Pili mwaka huu alitoka Mugumu Serengereti na kwenda kulipoti shuleni kidato cha kwanza katika sule ya Sekondari Mkuyuni iliyoko Manyara akiwa na kaka yake na alopokelewa shuleni hapo tarehe tano mwezi huo wa pili.
Tarehe Sita mwezi wa Tatu mwanafunzi huyo alitoweka ghafla shuleni hapo ambapo hakuondoka na chochote wala yoyote kufahamu taarifa za kupotea kwake.Juhudi za kumtafuta bado hazijazaa matunda, hivyo unaombwa kutoa ushirikiano wako kama utakuwa na taarifa zozote juu ya kijana huyu.
Mawasiliano ya Mzazi wake ni 0788 75 58 98 AU 0764 74 34 59 anaitwa Nsanda Joseph Mkazi wa Kenyana B, Mugumu Serengeti.
Mtoto anaetafutwa.Ukimuona tumia mawasiliano ya Mzazi wake ni 0788 75 58 98 AU 0764 74 34 59 anaitwa Nsanda Joseph Mkazi wa Kenyana B, Mugumu Serengeti.

No comments:

Powered by Blogger.