LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA KANDA YA ZIWA MAGHARIBI KUMEKUCHA. WANACHAMA WATAKIWA KUCHANGAMKA.

Tungaraza Njugu (Kushoto) ambae ni Kiongozi wa Oparesheni na Mwenyekiti wa Kamati ya Chadema ni Msingi Kanda ya Ziwa Magharibi. Kushoto ni Meshack Micus Michael ambae ni Afisa wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi.Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi inaundwa na Mikoa Mitatu ambayo ni Mwanza, Geita na Kagera.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi, kimewataka wanachama wake kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi ndani ya Chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi.


Hayo yameelezwa na Meshack Micus Michael ambae ni Afisa wa Chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari hii leo wakati wa kuelekea katika Uchaguzi wa Wilaya na Majimbo ndani ya Chama hicho unaotarajia kuanza hivi karibuni.


Michael amewasihi wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, badala ya kukaa na kulalamika kuwa hawapewi fursa na nafasi za kugombea zafasi za uongozi ndani ya chama chao.


Aidha amebainisha kuwa chaguzi za Majimbo na Wilaya unatarajia kuanza hivi karibuni na hadi kufikia Agost 10 Mwaka huu, chaguzi hizo zitakuwa zimekamilika na hivyo kuendelea na chaguzi nyingine katika ngazi ya za Mikoa.

Tungaraza Njugu.
Katika hatua nyingine amewataka Viongozi wa Chama hicho katika ngazi ya Kata, Wilaya na Majimbo, kuwahamasisha wanachama wao kujitokeza kwa wingi ili kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama chao.
Mbali na hayo Michael amebainisha kuwa kwa hivi sasa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi imetanuka Kiuongozi, kwa kuwa Chama Kimeunda kamati Sita ambazo ni kamati ya Sheria, Kamati ya Chadema ni Msingi na Kamati ya Fedha na Rasilimali.

Kamati nyingine ni pamoja na Kamati ya Sera na Utafiti, Kamati ya Hamasa na Uenezi na Kamati ya Mwisho ni Kamati ya Mafunzo ambapo Kamati zote sita zimelenga Kukijenga na Kukiimarisha chama hicho.

                                                                Meshack Micus Michael

Kwa Upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Oparesheni za Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi, amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuwa makini na dhana ya baadhi ya wanasiasa hapa nchini wanaosema kuwa Tanzania hivi sasa inahitaji Rais ambae ni Kijana na kuiita hoja hiyo kuwa ni Propaganda.

“Tumemsikia January Makamba akijitapa kwamba Watanzania sasa wanahitaji Rais ambae ni Kijana…hiyo hii ni Propaganda ambayo kimsingi nyuma yake hoja hii imekuja kutafsiriwa kwamba Makamba anampigia debe Benard Membe ambae amekuwa akizunguka kwenye matamasha mengi. Sasa kwa sababu Membe hawezi kusema, January anapewa Pesa anazunguka ili kumtanga Membe kwa namna ya Mgongo wa nyuma…” Alisema Tungaraza.

                                                                    Mwanahabari.

Katika Hatua nyingine kwa niaba ya Chama Tungaraza ameeleza kuwa chama kinasikitishwa na Kauli aliyoitoa hivi karibuni Waziri wa Ujenzi Mh.Dk.John Pombe Magufuli wakati akiwa katika Mikutano yake ya hadhara ambapo alisema kuwa Chama cha Mapinduzi CCM hakiwezi kuondoka Madarakani kwa njia ya Kura, kwa kuwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi na Viongozi wote ni makada wa CCM jambo linaloashiria kuwa wanakisaidia chama.

Kutokana na Kauli hiyo Tungaraza amebainisha kuwa wanataka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi NEC kueleza kama ni alichokisema DK.Magufuli ni sahihi, kwa kuwa kukaa kwao kimya inaashiria kwamba maneno aliyoyasema Dk.Magufuli ni sahihi kiasi kwamba hata ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa na Tume ya Uchaguzi kwa pamoja zinafanya kazi kwa matakwa ya CCM na si kwa misingi ya Sheria.

Waandishi wa Habari wakiwa katika Mahojiano na Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Kona ya Bwiru Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza..

Na: George Binagi @99.4 Radio Metro & Mtanzania Media Blog.

No comments:

Powered by Blogger.