LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBUNGE WA NYAMAGANA EZEKIEL WENJE, AINGILIA KATI OPERESHENI INAYOENDELEA JIJINI MWANZA.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje akiwahutubia wafanyabiashara ndogo ndogo Jijini Mwanza katika Uwanja wa Nyamagana. Aliekaa pembeni ni Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi Robert Bujiku.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.Ezekiel Wenje amesema kuwa Operesheni ya Kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo yasiyoruhusiwa Kisheria katikati ya Jijini Mwanza, Inapaswa kusitishwa mara moja utokana na Operesheni hiyo kutekelezwa pasipo kuzingatia Utu na Ubinadamu.Mh.Wenje ambae ni Mbunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, ametoa kauli hiyo hii leo Mkoani Mwanza wakati akizungumza na Wafanyabiashara hao maarufu kama Machinga, katika Mkutano uliofanyika katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana.

Akizungumza katika Mkutano huo, Wenje amebainisha kuwa yeye hakatai Machinga kuondolewa katika Maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria katikati ya Jiji la Mwanza, isipokuwa anapingana na namna Operesheni hiyo inavyoendeshwa ambapo Mgambo wa Jiji wamekuwa wakiwanyanyasa Wafanyabiashara hao pindi wanapokuwa wakitekelezwa Operesheni hiyo.

“Mimi Msimamo wangu sijakaa watu waondolewe Nyerere Road na Kenyatta Road, lakini hii Operesheni izingatie Ubinadamu..kwa nini Polisi apige mtu? Mtu anakamatwa anapigwa, Kuna mwanamke juzi nimeambiwa amekamatwa amepigwa kwelikweli na polisi…mpaka migambo, migambo wanatuzingua wakati jioni wanalala kwao bila bunduki…hata hawa polisi hawatembei na bunduki...kwa hiyo ninachosema tunahitaji amani iwepo katika huu mji…kwa hiyo hatuhitaji mwananchi hata mmoja anyanyaswe… ” Alisema Wenje.

Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi Robert Bujiku akizungumza katika Mkutano huo.

Mbali na hayo Wenye aliweka bayana maadhimio manne ambayo ambayo wanahitaji yafanyiwe kazi ili kuondoa manyanyaso yaliyotokana na Operesheni hiyo, ambapo miongi mwa maadhimio hayo ni pamoja na kukusanya majina ya watu waliokamatwa katika operesheni hiyo ili mchakato wa kuhakikisha wanaachiwa huru ufanyike mara moja.Pia amewataka wafanyabiashara hao kuweka sahihi zao kwa ajili ya kwenda mahakamani kufungua kesi ili operesheni hiyo isitishwe ikiwa ni pamoja na kuwaagiza madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupeleka hoja katika kikao kijacho cha halmashauri ya jiji la Mwanza kuhakikisha operesheni hiyo inasimamishwa na kama hilo litashindikana wawe tayari kususia kikao hicho.

                         Diwani wa Kata ya Mahina Jijini Mwanza  (Chadema) Charles Chinchibera.

Aidha ametoa rai kwa wale wote wenye ushahidi wowote kuhusiana na kuhusiana na mali zao kukamatwa pasipo kurejeshwa, wauwasilishe katika Ofisi za Kanda za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya kusaidia katika kesi ambayo inakwenda kufunguliwa kuhusiana na Operesheni hiyo huku akibainisha kuwa Chama kinakwenda kufungua kesi ambayo itaongozwa na jopo la Wanasheria wapatao watano akiwemo Gaspar Mwanalyela pamoja na Mh.Tundu Lisu


    Sahihi zilizowekwa kwa ajili ya kusaidia katika kesi inayotarajiwa kufunguliwa Mahakamani.

Awali akizungumza katika Mkutano huo, Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi Robert Bujiku amebainisha kuwa Operasheni inayoendelea katika Jiji la Mwanza ni Unyanyasaji Mkubwa ambao hata wanaotekeleza Oparesheni hiyo wasingeweza kuutenda kwa ndugu zao.


                         Tungaraza Njugu (Kulia) kiongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi. 
Nae Diwani wa Kata ya Mahina (Chadema) Charles Chinchibera amebainisha kuwa suala la Machinga katikati ya jiji la Mwanza limekuwa na mvutano mkubwa kutokana na Machinga kukosa maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao na badala yake maeneo hayo yamechukuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya watumishi wa halmashauri, maaskari na Makatibu Tarafa. 


Kwa upande wao baadhi ya Machinga waliokamatwa katika Operesheni hiyo wameelezea kusikitishwa kwao kulingana na namna Operesheni hiyo inavyoendeshwa, kwa kuwa wamekuwa wakikamatwa na kunyang’anywa bidhaa zao na hata wanapotakiwa kuzichukua huambiwa walipe faini ambayo ni zaidi ya thamani ya mali zao, huku bado wakiwa wamefunguliwa mashitaka mahakamani kwa kufanya biashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa.
''Kinachinisikitisha kuna mtoto anaekadiliwa kuwa na umri chini ya miaka 15 alikamatwa akiuza mikanda na betri za simu, wakamkamata na kumfikisha mahakama...alipoulizwa umekamatwa ukifanya biashara katika eneo ambalo haliluhusiwi, kwa kuwa hajui kitu akakubali, amefungwa miezi sita pale Butimba, sasa hiyo ni haki kweli...'''Alisema Wenje na kuongeza..

''Wanasema machinga wanachafua mji, hivi kati ya machinga na ile barabara ya pale Pamba ambayo wameshindwa kuitengeza na machinga nini kinachafua mji?...''

''Wao wanadhani wananikoma mimi...hawanikomoi mimi wanawakomoa Watanzania...''
Huyu ni Mmoja wa Machinga walioathirika na fujo za machinga dhidi ya Polisi Jijini Mwanza ambapo yeye alipigwa risasi na kuwa kama hivi unavyomuona sasa.                       Peopleeeeeeeeeee.......Powerrrrrrrrr

''Wenjeeeeee...Wenjeeee....Wenjeeeee...Wenjeee''
Na:George Binagi @Radio Metro & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.