LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WASHTUSHWA NA MAANDAMANO YA MOM'S YALIYOFANYIKA HII LEO.

Maandamano haya yamewashtusha wakazi wa jiji la Mwanza huku kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kujua nini kinachoendela. Yalikuwani Maandamano ya ambayo yameandaliwa na Muungano wa Akina Mama walio tayari katika maombi kutoka Katika Madhehebu yote ya Kikristo hapa nchini. Umoja huo umelenga Kuwaombea Watoto na Taifa kwa Ujumla ukiwa unafahamika kama MOM'S in Prayer. Huduma ya MOM'S in Prayer Iliingia hapa nchingi tangu mwaka 1992 ikitokea nchini Marekani na ilisajiriwa rasmi kisheria hapa nchini tangu mwaka 1995. Soma na Tazama picha.
Kongamano la Kitaifa la Akina Mama walioungana kwa ajili ya maombi kutoka Katika Madhehebu yote ya Kikristo hapa nchini, leo limeanza Mkoani Mwanza likiwa limelenga kuwaombea watoto na Taifa kwa Ujumla.
Kongamano hilo linafanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT  huku likiwa chini ya huduma inayofahamika kama MOM’S in Prayer ambao ni muungano wa Wamama hao kutoka Madhehebu yote ya Kikiristo hapa nchini.

Akizungumzia Kongamano hilo, Deborah Maisel ambae ni Katibu Mkuu wa MOM’S hapa nchini amebainisha kuwa, huduma hiyo ya MOM’S in Prayer iliingia hapa nchini tangu mwaka 1992 kutoka nchini Marekani na kusajiliwa rasmi kisheria mwaka 1995 ikiwa imelenga kutoa elimu ya mambo mbalimbali yakiwemo ya Kiroho na Kimwili.
Amebainisha kuwa Kongamano hilo la Kitaifa la MOM’S in Prayer hufanyika Mara Moja kila baada ya Miaka Miwili, hivyo mwaka huu linafanyika Mkoani Mwanza kuanzia leo Jumatano ya July 16 na linatarajia kufikia tamati Jumapili ijayo ya July 2o.
Anitha Lordvice Mamuya ambae ni Katibu wa Wamama kutoka Mkoani Kilimanjaro Usharika wa Longuo, amesema kuwa maombi ya Kongamano hilo zaidi yamelenga kuleta badiliko kwa ajili ya watoto kutokana na changamoto zinazowakabili katika jamii.
Watoto nao wakaungana na Akina mama hawa wa MOM'S in Prayer kwa kuwa watoto ndio wanaoguswa zaidi na Maombi ya Kongamano hili linalofanyika Kila baada ya Miaka Miwili hapa nchini likihusisha Muungano wa Akina mama kutoka katika madhehebu yote ya Kikristo hapa nchini.
Wamama hao wakiwa katika Kanisa Katoliki la Nyakahoja mara baada ya Kuhitimisha maandamano ambayo pia yalianzia Kanisani hapo na kupita katika barabara zote za katikati ya Jiji la Mwanza kabla ya kuelekea katika viunga vya Chuo Kikuu cha Saut ambako kongamano hilo la Maombezi linafanyikia.
Na:George Binagi @Radio Metro & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.