Binti alienusurika Kubakwa.
Mama mdogo wa Binti alietakwa kubakwa (Hakutaka Kuandikwa jiana lake)
ambae ndiye aliempeleka binti huyo kwa ajili ya kufanya kazi za ndani nyumbani
kwa Mtuhumiwa huyo, amesema kwamba binti huyo alimpigia simu jana (Jumapili) na kumpa
taarifa hizo ambapo mapema leo (Jumatatu) ameenda nyumbani hapo na kumkuta mama mwenye
nyumba ambae amekiri nae yeye kupokea taarifa za mfanyakazi wake kutaka
kubakwa.
“Mimi alinipigia Simu jana jioni (Jumapili) nikiwa nyumbani sasa nikasema usiku huu siwezi kwenda kumfuata ikabidi nilale hadi
asubuhi ambapo nimeenda leo (Jumatatu) asubuhi na kumkuta mama mwenye nyumba ambae
nae alieza kusikitishwa na tabia ya mme wake kwa kuwa hiyo ni mara ya pili
kuonyesha tabia ya aina hiyo kwa wafanyakazi wake wa ndani kwani hata mfanyakazi
aliekuwepo awali nae aliondoka nyumbani hapo kutokana na tabia hiyo”.
“Nilivyofika nyumbani sikumkuta huyo mwanaume (Mtuhumiwa) na hata
nilipompigia simu alipokea na kuanza kunifokea kuwa mimi niseme kama kuna kitu
kingine ninachokitafuta kutoka kwake maana hayo mambo yameisha na tayari
amemuomba msamaha (binti) hivyo kama kuna kitu kingine anachikitaka aseme
badala ya kumfuatilia” alisema mama mdogo wa binti huyo baada ya kwenda
kumfuata huyo binti.
Alipotafutwa mtuhumiwa huyo (Jina tunalo) kwa njia ya simu hii leo
(Jumatatu) ili kuelezea juu ya tuhuma anazopewa hakuwa tayari kuzungumza badala
yake alielekeza kuwa atafutwe mwanasheria wake ambapo alitoa namba za
mwanasheria wake ambaye katika msg aliyotuma jina la Mwanasheria huyo
liliandikwa “Makaza Advovate”.
Hatimae mwanasheria huyo alipigiwa simu na kujifanya hajui
chochote juu ya tukio hilo na baada ya kuelezwa na mwandishi wa habari hizi
kuwa taarifa hii ingeweza kutolewa bila upande wa pili kusikilizwa aliamua
kukubali kukutana na mwandishi wa habari hii katika ofisi alizoziita za kwake
japo hakukua na ishara yoyote ya kuonyesha kuwa ofisi hiyo ni ya wanasheria
iliyoko katika jengo la ECKACLIF Isamilo Jijini Mwanza ghorofa ya pili.
Mwandishi wa habari hizi alipofika katika jengo hilo la ECKACLIF
akiwa ameambata na mwenzake mmoja alikutana na mwanasheria huyo ambae alikuwa
na mwenzake katika ofisi hiyo na katika kuelezea tukio hili yeye alisema kuwa
ni bora mwandishi akaenda polisi kufungua mashtaka badala ya kupoteza muda
jambo ambalo haliwezi kusaidia chochote.
Baada ya Mvutano mrefu baina ya mwandishi wa habari hizi, akiwa na
mwenzake aliamua kutoka ndani ya ofisi hiyo ya mwanasheria wa Mtuhumiwa huyo bila kupata maelezo yoyote kutokana na tuhuma za tukio hizo,
huku mtuhumiwa akibainisha kwa njia ya simu kwamba maelezo yaliyotelewa na mwanasheria
wake ndiyo yako sahihi na hakuwa na cha ziada.
Busara za mwandishi ni kwamba vitendo hivi visipodhibitiwa katika
jamii, tutaendelea kushuhudia watoto wetu wakipitia manyanyaso makubwa ya
kiukatili katika jamii zetu. Hili suala sasa haliko chini ya Mwandishi tena
bali yeye amelileta katika jamii kwa imani kwamba Wanaharakati wanahusika na
utetezi wa Haki za Watoto, Haki za Wanawake ama Haki za Binadamu wanaweza
kulifuatilia suala hili kwa kina zaidi.
USIKOSE KUFUATILIA CHAPISHO LIJALO JUU YA TAARIFA HII.
|
No comments: