LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU CCM AONGOZA UTAMU WA MWEZI MTUKUFU.

Katibu Mkuu wa CCM Mh.Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wageni waliohudhuria Futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM, MNEC Mh.Christopher Mwita Gachuma. 

Hafla hiyo ilifanyika Katika Ukumbi wa Roof Top ndani ya New Mwanza Hotel jana Jumamosi na iliambatana sanjari na Sala ya Magharibi ndani ya Ukumbi huo ambapo Waislamu na Wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, vyama vya siasa na Serikali walihudhuria. 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Salim Hassan.
MNEC, Mh. Omary Christopher Mwita Gachuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika Hafla hiyo ya Futari ambapo zaidi alisisitiza juu ya Suala la Amani kudumishwa katika Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa Ujumla kwa kuwa amani ndio msingi wa kila kitu.
       Mh.Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu CCM.
   Hatimae zoezi lenyewe likawadia....ilikuwa ni pakua...Pakia....Tizama Picha mwanawane..
 
 
 
 
Ahsante kwa kuungana nasi, hakika umeshuhudia Utamu wa Mwezi Mtukufu, Utamu ambao ni Kushiriki Futari na Wanajamii wenzako jambo ambalo husaidia katika kuongeza Baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Na: George Binagi @99.4 Radio Metro & Binagi Media Group

No comments:

Powered by Blogger.