LIVE STREAM ADS

Header Ads

LIL STIGGAR KUZINDUA MIXTAPE YAKE YA RISE AND SHINE NDANI YA MTENDA SUNSET.

Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kukupita katika maisha yako lakini usijutie hata siku moja. Lakini pia yapo mambo ambayo yakikupita lazima ujutie, na mambo hayo mara nyingi ni yale yanayotokea mara moja baada ya muda mrefu/ si mambo ya mara kwa mara...Sasa uzinduzi wa Mixtape ya Rise and Shine ya Msanii Lil Stiggar ni moja ya matukio ambayo hutakiwi kukosa maana utajuuu......Utajuuu....Malizia mwenyewe.

Rise and Shine Mixtape ni Kanda Mseto ya Mwanamziki Lil Stiggar inayosubiriwa na Mamilioni ya Watanzania, ambayo imebebwa na vionjo mbalimbali vyenye kukonga nyoyo za mashabiki lukuki.

Dhahiri Shairi muziki unadaiwa kuwa ni moja ya Tiba kwa wagonjwa bada ya watafiti kadhaa nchini Marekani kuwaweka wagonjwa 100 katika chumba chenye muziki na wengine 100 kupelekwa hospitalini, lakini waliowekwa katika chumba maalumu chenye muziki walionekana kupona mapema, kwa mantiki hiyo basi kanda mseto ya RISE & SHINE ya LIL STIGGAR ni dozi tosha.

Mwanamziki LIL STIGGAR ni msanii anaetokea Kundi la Umoja wa Wasanii wa Kike nchini Tanzania liitwalo FeMCTZ ambalo linaundwa na wasanii wengine kama vile Cindy Rulz, Stosh, Tamy, Tiffer, Natty E na Kiongozi wao Chiku K.

Kuhusu Kanda Mseto ya Rise anda Shine ya Lil Stiggar ni kwamba itakuwa na jumla ya Nyimbo Saba na Bonus Trucks, sanjari na Shows mbalimbali alizowahi kuzifanya Lil Stiggar, video/nyimbo zake, lylics pamoja na Biography yake ambavyo vyote kwa pamoja vitakuwa katika mfumo wa DVD.

Wasanii walioshirikishwa katika Kanda Mseto hiyo ni pamoja na Phyno, Ammy Chiba, Gest Lydar, Chris Daniel, Ottuck, Zax B, Sauti from East na Anno Melody. Maprodyuza waliohusika kuitengeneza Rise and Shine Mixtape ni Phyno Touchz, Dayo Music, MG Creator, Losso Touchez, Gach, Nachi & Waisa, Kingston na Kebby.

Uzinduzi wa Rise and Shine utafanyika Agost 02 Mwaka huu Jiji Mbeya katika Ukumbi wa Mtenda Sunset Conference kwa Kiingilio cha Shilingi 10,000 ambapo tiketi zimeanza kuuzwa hivyo wahi mapema kununua tiketi yako mapema kupitia Simu namba 0654 07 99 30.
Uzinduzi huo utasindikizwa na Wasanii kibao huku Red Carpet, Dancing na Maonyesho ya Mavazi ya Kiafrika yaliyopewa jina la "SONDELA".Uzinduzi huu umedhaminiwa na Bomba FM Radio, Mbeya FM, The Premier Show ya G FM, Life Parners Ent, Sweet FM, Highlands FM, T Motion Films, Elishadai Records, Native Films, Chimbuko letu Blog na Kuletwa kwenu na Mtanzania Media Blog.

NB: Unaweza Like page ya Lil Stiggar kupitia facebook kwa jina hilo la LIL STIGGAR na Instagram kupitia jina hilo pia la LILSTIGGAR.
Na: Greyson Salufu Chatanda a.k.a Chris Bee-Mbeya.

No comments:

Powered by Blogger.