MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014 KUKABIDHIWA ZAWADI ZAKE SIKU YA JUMAMOSI.
![]() |
Hongera sana Bahati Muriga, Mama Shujaa wa Chakula 2014, Hakika huu ni Ushindi kwa Wanawake wote kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa. |
Wageni kutoka Shirika la KIVULINI na Oxfam wakiwa katika Studio za Metro FM Jijini Mwanza. |
Bahati Muriga Mwenyeji wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza ambae ni Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2014, anatarajiwa Kukabidhiwa zawadi zake Jumamosi hii ya October 02 Mwaka huu huko Wilayani Ukerewe.
Muriga alijishindia zawadi mbalimbali ambazo ni Vifaa vya Kilimo ambavyo vina thamani ya Shiling Milioni 25 baada ya kuibuka Mshindi wa Shindano hilo la Mama Shujaa wa Chakula 2014 kwa Kuwamwaga washiriki wenzake katika Mchuano ambao ulikuwa Mkali kweli kweli.
Hadija Liganga Kutoka Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI lenye Makao yake Mkoani Mwanza. |
Washiriki
walioshiriki shindano hilo ni MS Elinuru M. Pallangyo - Arusha, Dorothy
D. Pallangyo - Arusha, Leah D. Mnyambugwe - Dodoma, Martina G. Chitete -
Iringa, Grace G. Mahumbuka - Kagera, Zinaida J. Kijeri - Kigoma, Upendo
M. Msuya - Kilimanjaro, Neema U. Kivugo - Manyara, Elizabeth Simon -
Morogoro, Joyce N. Hassan - Mtwara, Bahati Muriga - Mwanza (Mshindi), MS
Thereza Kitinga - Mwanza, Santina Mapile - Njombe, Mary A. Ndasi -
Rukwa, Fredina M. Said - Shinyanga, Esther Kulwa - Simiyu, Mary J.
Mwanga - Singida, Doricus M. Shumbi - Singida, Kuruthum R. Mwengele -
Tanga.
Lengo
la kuanzishwa kwa Shindano hilo la Mama Shujaa wa Chakula ni kwa ajili
ya kuwahamasisha akina mama kote nchini kujikita katika Kilimo kwa ili
kuweza kujikwamua na umaskini sanjari na Utegemezi katika familia huku
shindano ambapo shindano hilo limekuwa likidhaminiwa na Shirika la OXFAM
huku likiamini katika kuwekeza kwa Wakulima wadogo wadogo wanawake kwa
kuwa Inalipa.
No comments: