LIVE STREAM ADS

Header Ads

MOJA HAIKAI. MBILI NAYO IMEGOMA. KISA SIKU KUU YA EID.

Mishe Mishe Katika Mtaa wa Makoroboi Jijini Mwanza Zikiendelea hii leo.
Leo ni Mapumziko ya Siku kuu ya Eid, Watanzania wameungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwa ajili ya Mapumziko na Kusherekea kwa pamoja siku hii mhimu kwa ndugu zetu Waislamu. Kama ujuavyo kila jambo lina Neema zake. Sikukuu hii imekuwa ni Neema kwa Baadhi ya Wafanyabiashara Jijini Mwanza ambao wamezungumza na Mtanzania Media.

Katika Mtaa wa Makoroboi  na Mtaa wa Msikiti wa Ijumaa Jijini Mwanza baadhi ya Wafanyabiashara waliozungumza na Mtanzania Media wanasema kuwa kuwa Sikukuu hii imekuwa Neema kwao kutokana na biashara zao kuchanua katika Msimu huu.

Asilimia kubwa ya wafanyabiashara waliopata Neema hii ni pamoja na wale wanaouza nguo za aina mbalimbali, sanjari na wale wanaouza bidhaa mbalimbali kama vile Nafaka. Msomaji wetu jionee mwenyewe pilika pilika ilivyokuwa mapema leo Jijini Mwanza. Kwa wale wenye FAMILIA tunasema MOJA HAIKAI.MBILI NAYO IMEGOMA. KISA SIKU KUU YA EID maana hapo mfuko Pochi lazima ilegee tu. Lakini usijali ndio Utu uzima huo. MTANZANIA MEDIA INAKUTAKIA EID NJEMA.
Mishe Mishe Katika Mtaa wa Makoroboi Jijini Mwanza Zikiendelea hii leo.
Jambo la Mhimu ni kwamba Kila Mwislamu anapaswa kumshukuru mola wake kwa kusema “Alhamdulillah” kumwezesha kuifunga ramadhani kwani wapo wengi ambao wangependa kutekeleza ibada hii, lakini hawakuweza kwa matatizo mbalimbali yakiwamo magonjwa, vita, vifo, ajali na majanga ya njaa na ukame.
 
Huu ni wakati wa waumini wa dini ya Kiislamu nchini kuungana na wenzao duniani kote kusherehekea sikukuu hii ya Idd El Fitri baada ya kukamilisha ibada kongwe ambayo pia iliwajibishwa na kutekelezwa na watu (umma) waliowahi kuishi katika hii dunia kabla ya Muhammad (S.A.W). 

Siku ya Idd ni siku ya kuwaangalia kwa jicho la huruma wagonjwa waliomo majumbani na hata hospitalini, wafungwa magerezani kwa kuwatembelea na kuwasaidia kwa kila hali sambamba na kuwaombea dua ya kuwatakia afya njema, nusura ili wamshukuru Mwenyezi Mungu na wajione ni sehemu muhimu katika sherehe hii.



Ni siku ya Waislamu kupongezana kwa kumaliza mfungo wa Ramadhani kwa kuwa ndio lengo la kuifuatishia kwa zaka ya chakula muhimu kinachopendwa katika mji au jamii husika ambacho kwa Tanzania chakula hicho ni mchele.
 

George Binagi @Radio Metro & Mtanzania Media (Kulia) akizungumza na Wakazi wa Jiji la Mwanza Eneo la Msiki wa Ijumaa hii leo.


Ama wale ambao watafanya fujo katika siku hii wakidhania kwamba ndio wamefika na wakaamua kuzikomoa swaumu zao kwa matendo maovu, hao watakuwa na tathmini mbovu na watakuwa wameshinda njaa tu lakini hawakufunga, kwani funga humwandaa mtu kuwa mcha Mungu.

Ni siku ya kuiendeleza ahadi uliyoichukua ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kama uliipenda swala, kusoma Quran, kusimama usiku, kukaa itikafu, kukirimu watu, kusaidia wanyonge, kuhurumia wasiojiweza na ukachukia zinaa, dhuluma, rushwa, kusengenya, kusema uongo, kunywa pombe na kuiba.
Miongoni mwa mambo ambayo ni muhimu kwa Muislamu kuyafanya siku ya Idd kama yalivyofanywa na kusisitizwa na Kiongozi wa Umma, Mtume Muhammad (S.A.W) ni kutoa zakatul fitri na kupata kifungua kinywa kabla ya kuswali swala maalumu ya Idd, kubadili njia wakati wa kwenda au kurudi kuswali Idd, kuswali Idd viwanjani na siyo msikitini.

Picha zote kushuka chini ni George Binagi @Radio Metro & Mtanzania Media (Kulia) akizungumza na Wakazi wa Jiji la Mwanza Eneo la Msiki wa Ijumaa hii leo.


Kila Muislamu anapaswa kuweka akilini kwamba Sikukuu ya Idd ni siku ya kutubia na siyo kutibua, ni siku kushukuru na siyo kukufuru, ni siku ya kuhurumiana na siyo ya kutesana kwa uadui, ni siku ya kupendana kwa ajili ya Allah na siyo ya kuchukiana, ni siku ya kutembeleana na siyo ya kukimbiana, ni siku kusalimiana na kujuliana hali na siyo ya kutukanana, ni siku ya kusuluhishana migogoro na siyo ya kufufua na kuanzisha migogoro mipya au kugombana, naam ni siku ya furaha na kuombeana kheri na siyo mabaya.

George Binagi @Radio Metro & Mtanzania Media (Kushoto) akizungumza na Mmoja wa Wafanyabiashara wa Eneo la Makoroboi wa Jijini  Mwanza.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.