Kwa Wakazi wa Jiji la Mwanza watakuwa wanajiuliza Maswali mengi kuhusiana na ile Show ya African Night (Usiku wa Mwafrika) ambayo imepangwa kufanyika tarehe 01.08.2014 Katika Ukumbi wa Serengeti pale JB Belmont Hotel na Suku ya tarehe 02.08.2014 pale Buzuruga Plaza.
Sasa iko hivi, Kamata huu Mtonyo kutoka Mtanzania Media ambayo imeshuhudia Mpango mzima kuhusiana na Show hiyo. Ni kwamba leo Utepe umekatwa rasmi kuhusiana na Show hiyo ambayo itakuwa ya kipekee miongoni mwa Shows ambazo zimewahi kufanyika Mkoani Mwanza.
 |
Afisa Masoko JB Belemont Suleiman Kupaza (Kushoto) akizungumza juu ya Shows za Usiku wa Mwafrika. |
Kwanza unapaswa kufahamu kuwa shows hizo zitakuletea burudani za
Kiafrika, Misosi ya Kiafrika na Mavazi ya Kiafrika ambapo
atakaetokelezea Kiafrika atapata Zawadi. Jukwaani sasa ndipo kutakuwa na
kasheshe, Hapa Saida Karoli pale Osogo Owinyo huku wakisindikizwa na
Madancers wakali kutoka nchini Kenya ambayo wanafahamika kama
Chipukizi.Com
Hakika itakuwa balaa ikizingatiwa kwamba
kiingilio itakuwa ni sawa na bure ambapo Show ilivyoandaliwa.
Pale JB Belemont Hotel VIP watalipa 20,000 na Viti vya kawaida itakuwa
10,000 huku pale Buzuruga Plaza kiingilio ikiwa ni 10,000.
Akizungumzia Shows hizo hii leo, Afisa Masoko kutoka JB Belmont Hotel Suleiman
Kupaza amebainisha kwamba maandalizi yote yamekwisha kamilika ikiwa ni
Pamoja na Wasanii watakaotumbuiza katika Shows hizo kuwasili Jijini
Mwanza na hivyo kuwasihi wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji jirani
kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya kukata na shoka itakayodondoshwa siku hiyo ya Tarehe 01.08.2014 na tarehe 02.08.2014 ambapo
Milango itaanza kufunguliwa mapema kabisa kuanzia majira ya saa moja jioni katika shows zote
kwa maana ya JB Belmonr na Buzuruga Plaza.
 |
Hawa ni Wasani kutoka nchini Kenya ambao wanafahamika kama Chipukizi.Com |
 |
Hawa ni Wasani kutoka nchini Kenya ambao wanafahamika kama Chipukizi.Com |
 |
Chipukizi.Com kutoka nchini Kenya |
 |
Chipukizi.Com wako tayari kwa ajili ya Shows hizo. |
 |
Huyu ndie Event Cordinatore mwenyewe, anafahamika kama Moses Manta. |
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.
No comments: