LIVE STREAM ADS

Header Ads

MASANJA MKANDAMIZAJI SASA AIVA. AWEKA BAYANA UKWELI WAKE KUHUSU HUDUMA YA UTUMISHI WA MUNGU.

Waimbaji wa Nyimbo za Injili Emmanuel Mgaya aka Masanya Mkandamizaji (Kushoto) akiwa na Samwel Lusekelo (Kulia) ndani ya Studio za Metro FM Jijini Mwanza mapema leo asububuhi (Jumapili) katika Kipindi cha Metro Gospal Time na Delphina Kyaruzi. Katika Mazungumzo yake ndani ya Kipindi hicho Masanja ameweka bayana kuwa hivi sasa siyo Mchungaji Mtarajiwa tena bali ni Mchungaji kamili.
Waimbaji hawa wako Mkoani Mwanza kwa ajili ya Kuhudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili Unaofanyika katika Uwanja wa Furahisha Wilayani Ilemela. Mkutano huu ulianza tangu Jumapili ya wiki iliyoisha ya June 29 na unatamatishwa hii leo July 06. Katika Mkutano huo, mbali na huduma ya Uimbaji pia Masanja anahudumu kama mchungaji hivyo kama jana jumamosi hukumshuhudia akihubiri katika Uwanja wa Furahisha, basi leo hutakiwi kukosa kwa kuwa Masanja atakuwa akihudumu katika Mkutano huo. Pia mwimbaji Flora Masha nae atakuwepo katika Mkutano huo.
Kwa taarifa tu kama ulikuwa hujui Masanja anahudu kama Mchungaji katika Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Jijini Dar es salaam, chini ya Bishop Bruno Mwakiborwa.
Joshua Dede ambae ni Mtangazaji wa Kwa Neema Radio ya Jijini Mwanza akiwa katika Studio za Metro Fm ambae alikuwa ameambatana na waimbaji hao. Ahsante kwa Kutembelea Mtanzania Media....Tukutane Furahisha kwa ajili ya Kupokea baraka za bwana katika Mkutano huo wa Injili ambao unafanyika katika Uwanja huo.Shukurani kwa Kanisa la EAGT City Centre Jijini Mwanza Chini ya Mchungaji Michael Kulola kwa kuandaa Mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.