LIVE STREAM ADS

Header Ads

MCHUNGAJI MASANJA MKANDAMIZAJI ALIVYOLIPUA MAPEPO KATIKA UWANJA WA FURAHISHA MKOANI MWANZA.

Baada ya kuweka bayana kuwa hivi sasa siyo Mchungaji Mtalajiwa bali ni Mchungaji Kamilili, Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji jana amepiga neno la Mungu katika Uwanja wa Furahisha Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza ikiwa ni katika Kutamatisha Mkutano Mkubwa kabisa wa Injili uliodumu kwa takribani wiki nzima kuanzia Jumapili June 29 hadi jana July 06. 2014.
Mkutano huo uliandaliwa na kanisa la EAGT City Centre Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Michael Moses Kulola. Mbali na Masanja kuhubiri na kuimba pia walikuwepo waimbaji mbalimbali kama vile Samwel Lusekelo na Frola Mbasha. Tazama picha jinsi Umati ulivyolipuka katika Mkutano huo japo tumeshindwa kuonyesha picha za picha za watu waliolipuka mapepo kutokana na sababu za kimaadili lakini kubwa zaidi ni kwamba watu wengi waliponywa sana katika Mkutano huo.

Kwa taarifa tu kama ulikuwa hujui Masanja anahudu kama Mchungaji katika Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Jijini Dar es salaam, chini ya Bishop Bruno Mwakiborwa.













Ahsante kwa kutembelea Mtanzania Media.....Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha unapata habari na matukio mbalimbali kadri tunavyoyapata.Tunakuomba U-LIKE ukurasa wetu wa Mtanzania Media Kwenye Facebook ili kuungana na Familia hii kubwa kabisa.

No comments:

Powered by Blogger.