LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOKO LA BUGARIKA JIJINI MWANZA LAWAKA MOTO.

Soko la Bugarika lililoko Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza limewaka Moto Usiku huu (Jumamosi) majira ya saa nne na kuteketeza baadhi ya Bidhaa na Mali za Baadhi ya Wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika Soko hilo.Chanzo cha Moto huo kimeelezwa kuwa ni Shoti ya Umeme huku taarifa kutoka jeshi la zima Mototo Mkoani Mwanza zikieleza kuwa ni Mlipuko uliotokana na Mafuta ya Petrol yaliyokuwa yakiuzwa katika duka lililokuwa jirani na soko hilo na juhudi za kuuzima moto huo zimefanikiwa kwa ushirikiano na wananchi pamoja na Kikosi cha Zima Moto na hivyo kusaidia kuuzima moto huo.Hakuna madhara makubwa yaliyosababishwa na moto huo kwa kuwa mali nyingi zimeokolewa katika soko hilo japo watu wawili (Mtu na Mke wake, wamiliki wa duka) waliokuwa katika duka ambalo moto ulianzia wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospital ya Bugando kwa ajili ya matibabu.
Ipo haja ya Suala hili la Masoko kuwaka moto kufuatiliwa kwa ukaribu ili kujua chanzo chake kwa ajili ya kudhibitiwa mapema, maana taarifa za masoko kuwaka moto sasa hapa nchini zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara huku asilimia kubwa ikielezwa kuwa husababishwa na akina baba/ mama ntilie ambao huacha majiko yao yakiwa na moto katika maeneo hayo.
Mtanzania Media inawapa pole wale wote waliokumbwa na tukio hili.Picha zote na Frank M.Joackim jicho letu kutoka eneo la tukio.

No comments:

Powered by Blogger.