LIVE STREAM ADS

Header Ads

AIRTEL YADHIHIRISHA KUWA BADO NI BABA LAO. YAVUNJA REKODI KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA ZIWA.

Hili lilikuwa ni Moja ya Mabanda ya Airtel katika Maonyesho ya Nane Nane ambayo yalifanyika Nyamhongolo Mkoani Mwanza ambapo
hiyo ilikuwa ni Kikanda kwa Maana ya Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Geita. Katika Kilele cha Maadhimisho hayo Kanda ya Ziwa kilichofanyika jana Octoba 08, 2014 Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Mizengo Peter Pinda. Pia Pinda alitunukiwa Tuzo ya Mkulima bora katika maonyesho hayo ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali maarufu kama maonyesho ya Nane Nane.
Katika Maonyesho hayo Makampuni mbalimbali yalionyesha Bidhaa zao huku Kampuni ya Simu Airtel ikionekana kivutio zaidi katika Maonyesho hayo kwa huduma ilizokuwa ikizitoa lakini zaidi
katika burudani iliyotolewa katika Jukwaa la Airtel.
 
 
 
Baada ya Wanainchi Kuhudumiwa sanjari na kujionea bidhaa mbalimbali za Airtel, Ukawadia ule wasaa wa Maburudani. Kiukweli palikuwa hapatoshi. Hilo nyomi sasa, ikawa ni balaa tupu. Watu walifurahi kile ambacho Airtel walikuwa wamekiandaa kwa ajili yao. Tazama Picha za Show iliyopigwa jana katika Maonyesho hayo ya Nane Nane katika Viwanja vya Nyamhongolo Mkoani Mwanza ambapo hii ilikuwa ni Katika Kanda ya Ziwa.
Hapa wanatafutwa wanaojua kudance...ilikuwa balaaaaaa.
 
Kiduku sasa hiiiiiiiii.
 
 
 
 
 
Eeeebwanaweeeeeeeee
Hatimae ukawadia wasaa wa Msanii Vice Kutoka Jijini Mwanza.....Ni Noumaaaaaa.
 
 
 
 
Mc. Darad-Mzee wa Kikombe nae alikuwa na amsha amsha za hatariiiii.
 
 
 
 
"SEMAAA AIRTEL....AIRTEL...AIRTEL...AMSHA AMSHA ZA HATARI"

"AIRTEL NI BABA LAOOOO" HATOKI MTU HAPAAAA"
 
Mc.Darada na Dancers Wake....Ni hatari tupu.
Hawa watoto wanacheza ni balaaa....Kanga Moko wanakaa nadhani hapa.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.