LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA MKOANI MWANZA NI KILIO NA MAJONZI. WAOMBA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KUWASAIDIA.

Picha ya Pamoja kati ya Wawakirishi wa Vijana Jijini Mwanza, Viongozi wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani Mwanza, Mwanza Youth and Children Network (MYCN) na Wawakirishi wa Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji Mwanza.
Kupitia Mradi wa Jiji langu Sauti yangu unaoendeshwa na Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza wa Mwanza Youth and Children Network (MYCN), Vijana Mkoani Mwanza wamepaza sauti zao na kuomba uundwaji wa baraza la Vijana ufanyike haraka iwezekavyo ili
kupata chombo kitakachotambulika kisheria ili kuwaunganisha katika masuala mbalimbali ya kimendeleo.

Wakizungumza hii leo katika Kikao baina yao na Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halimashauri ya Jiji la Mwanza, baadhi ya wawakilishi wa Vijana kutoka Jijini Mwanza wamebainisha kuwa, kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiomba uundwaji wa baraza la Vijana lakini ombi hilo limekuwa halitiliwi maanani licha ya utayari walio nao.
Vijana hao wameeleza kuwa kama uundwaji wa Baraza la Vijana Mkoani Mwanza na Taifa kwa ujumla utafanikiwa na kutambuliwa Kiserikali, Vijana watapata fursa ya kuwa na chombo kitakachokuwa kikiwaunganisha pamoja katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambayo ni pamoja na kupata fursa ya kukopesheka kupitia fedha zinazotengwa kwa ajili ya kuwasaidia vijana kujikwamua kimaendeleo.

Katika Kikao hicho, vijana hao wameiomba Halimashauri ya Jiji la Mwanza kuwapa ushirikiano wake wa hali na mali katika kufanikisha dhana nzima ya uundwaji wa baraza la Vijana Mkoani Mwanza, huku wakishauri kuwa suala hilo likifanikiwa Viongozi watakaochaguliwa katika baraza hilo wapate nafasi ya kushiriki masuala mbalimbali yanayowahusu vijana.
Wakizungumza kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Juliana Marcel ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Mfuko wa Vijana na Haika Temu ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wote kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wamewaahidi vijana hao kuwa ombi lao la kuomba uundwaji wa baraza hilo la Vijana Mkoani Mwanza watalifikisha katika ngazi inayohusika kwa ajili ya hatua za utekelezaji zaidi.

Juliana Marcel ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Mfuko wa Vijana (Kulia) akiwa na Haika Temu ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (Kushoto) na wote wanatoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Brightius Titus ambae ni Katibu Mkuu MYCN.
Jesica Jackel ambae ni Afisa Mipango MYCN.

Wawakilishi wa Vijana Mkoani Mwanza.

Wawakilishi wa Vijana Mkoani Mwanza.
Wawakilishi wa Vijana Mkoani Mwanza.
Wawakilishi wa Vijana Mkoani Mwanza.
Wawakilishi wa Vijana Mkoani Mwanza.
Wawakilishi wa Vijana Mkoani Mwanza.
Picha ya Pamoja kati ya Wawakirishi wa Vijana Jijini Mwanza, Viongozi wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani Mwanza, Mwanza Youth and Children Network (MYCN) na Wawakirishi wa Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji Mwanza.
Na: George Binagi @99.4 Metro MF & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.