LIVE STREAM ADS

Header Ads

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHOMWA KISU TUMBONI. UTUMBO NUSRA UMWAGIKE NJE.



Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza SACP. Valentino Mlowola.

Bernald Otieno (26) mkazi wa butimba kona  mtaa wa Magereza Mkoani Mwanza, amenusurika kifo baada ya mzazi mwenzake Martha Gabriel (32) kumchoma kisu tumboni.

Tukio hilo lilitokea
juzi jumanne saa nne usiku huko butimba ambapo Benard alidai kuwa alienda kwa ndugu zake Mtaa wa Igogo  siku ya jumapili kusalimia, akachelewa kurudi nyumbani kutokana na usafiri usiku huo  ulikuwa wa shida  akurudi nyumbani jumatatu.

Alisema kuwa siku hiyo alinimtaarifu mzazi mwenzake amekosa usafiri lakini hakumjibu kitu na siku ya jumatatu usiku alishangaa kuona mzazi mwenzake  amekusanya nguo zake kwa lengo la kutaka kuondoka nyumbani hapo.

‘’usiku huo tulikuwa tumelala na ghafla Martha aliamka na kuchukuwa kisu na kasha kunichoma tumboni ndipo nilijaribu kupambana nae na hatimae nikafanikiwa kutoka nje kwa lengo la kuomba msaada kwa majirani ambapo yeye nilimfungia  mlango kwa nje ili asitoke’’. Alisema Otieno.

Aliongeza kuwa Martha si mara yake ya kwanza kumfanyia kitendo cha kikatili na kipindi cha nyuma wakiwa wanaishi Mkoani Tabora aliwahi kumwagia mafuta  ya diesel na kumchomea nyumba alipokuwa amelala na watoto wake.

Mweyekiti wa mtaa huo Abeid Musa akizungumzia suala hilo amesema kuwa alisikia mtu anapiga kelele ya kuomba msaada na walipofika walimkuta Otieno kashikilia utumbo huku analia na hivyo wakamchukua na kumpeleka hospital ya Rufaa Bugando kwa ajili ya Matibabu zaidi.

Muuguzi kiongozi wa wodi Ester Pastor aliyempokea Otieno alisema kuwa kisu alichokuwa amechomwa kilikuwa kimepita hadi kwenye utumbo mwembamba hivyo ilibidi wamfanyie upasuaji na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

Kamanda wa Polisi Mkaoni hapa  SACP. Valentino Mlowola  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na amebainisha kwamba mtuhumiwa  huyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani muda wowote upelelezi utakapokamilika ili kujibu shitaka linalomkabiri.
Na Prisca Japhes: Mtanzania Media-Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.